23 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

JPM ahutubia kwa Kiswahili dhifa ya taifa

Rais Dk. John Magufuli(kulia), akipiga ngoma na mgeni wake Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, baada ya kuwasili  Ikulu jana. Dar es Salaam.
Rais Dk. John Magufuli(kulia), akipiga ngoma na mgeni wake Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, baada ya kuwasili Ikulu jana. Dar es Salaam.

NA FARAJA MASINDE, DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli, amehutumia kwa lugha ya Kiswahili katika hafla ya dhifa ya kitaifa aliyomwandaliwa Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ambaye alikuwa nchini kwa ziara ya mbili.

Alisema lengo la kutumia lugha hiyo ni kuikuza na kukitangaza Kiswahili kama  lugha mama ya taifa.

Hafla hiyo ilifanyika Ikulu  Dar es Salaam jana na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Rais mstaafu Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan  na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Katika ziara hiyo, Tanzania na India zilisaini mikataba ya miradi ya maendeleo katika sekta za maji, kilimo, viwanda, teknolojia ya habari na mawasiliano na afya katika kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili  kusaidia wananchi wake.

Mikataba hiyo ilisainiwa na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi baada ya kumalizika   mazungumzo na Rais Magufuli.

Mikataba iliyosainiwa ni ya mradi wa kusambaza maji katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam, mradi wa kusambaza maji Zanzibar wenye gharama za Dola za Marekani milioni 92.  Mradi huo unatarajiwa kufikia miji 17 nchini.

Mikataba mingine ni   unaohusisha mafunzo ya ufundi yatakayosaidia kuzalisha wataalamu mbalimbali ambako Waziri Mkuu, Modi  alisema utasaidia    kuimarisha uhusianao kati ya nchi hizo mbili.

Waziri Mkuu Modi alisema  Serikali ya India itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuongeza wigo wa biashara na hatimaye kukuza uchumi wa nchi hizo.

Naye Rais Dk. John Magufuli, alisema Serikali India imekua na ushirikiano mzuri na Tanzania hasa katika masuala ya maendeleo na imeweza kuwekeza nchini   dola za Marekani bilioni 2.4 na kuzalisha  ajira 54,176.

Alisema baadhi ya misaada iliyotolewa na Serikali ya India ni pamoja na  mashine ya vipimo vya   saratani katika Hospitali ya Bugando.

India pia imeahidi kuanzisha viwanda vya kutengeneza dawa za binadamu  zitakazotibu   magonjwa mbalimbali ikiwamo malaria, figo na kisukari,  na kutengeneza vifaa tiba vitakavyotumika katika hospitali mbalimbali nchini.

Rais Magufuli  alisema   India ina uhitaji mkubwa wa mazao ya kilimo hasa jamii ya kunde hivyo akawataka wakulima kutumia fursa hiyo kuzalisha mazao hayo kwa wingi.

“India ina uhitaji wa tani 200 za mazao jamii ya kunde, wakulima mnatakiwa kuzalisha mazao hayo kwa wingi kwa vile tayari kuna soko la uhakika, na tutahakikisha madalali hawatakuwapo ili mkulima asikandamizwe,” alisema Rais Magufuli.

Katika sekta ya uwekezaji nchini, India ni nchi ya tatu kwa uwekezaji Tanzania ikifuatiwa na Uingereza   na China.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles