Na KYALAA SEHEYE
UKUMUANGALIA tu lazima ucheke kwani ni kipaji na sio ngekewa, amefanikiwa kuteka watoto, vijana, watu wazima na wazee hiyo yote ni kutokana na kuigiza nyanja zote tena bila wasiwasi wowote ule, Lucas Mhavile maarufu Joti alitamba na Original Comedy kundi ambalo lilitoa burudani kwa muda wa miaka 11 bila kuwa na mpinzani katika angaza za uchekeshaji wenye mafundisho.
Kwa sasa kampuni yao imepumzika na kila mmoja kufanya shughuli zake ili kutoa fursa kwa vizazi vipya kuonyesha kazi zao, Kwa upande wake Joti ameamua kutumia mapumziko yake kwa kuanzisha Yotube Tv akiamini sasa hivi dunia iko kwenye kiganja.
“Nimeamua kuanzisha Yotube Tv kwa sababu dunia iko kwenye kiganja watu wanakosa muda wa kuangalia Tv, ila akiwa na simu yake ya mkononi anawez kuona chochote kile anachotaka hata kama ni saa sita usiku akiwa kitandani uwezo wa kumuangalia Joti upo.”
Tv hiyo imelenga nyanja zote na imeangalia sana watoto kwa sababu kitu akikipenda mtoto basi na mzazi atakipenda, pia kutoa elimu kwa watoto katika uchekeshaji wangu huo nitatoa elimu kwa watoto na mambo mengine mengi makubwa ya watoto yanakuja.
Watoto ni watu ambao wanaupendo wa kweli hawana unafiki na ndio vipaji ambavyo vinatakiwa kuendeleza kwa kuliona hilo nikaona hamna haja ya kuacha vipaji vyenye upendo wa kweli vipotee ni bora niwe navyo bega kwa bega.
“Licha ya kuegemea zaidi katika vipindi vya watoto, nitakuwa na vipindi vya watu wa rika zote pia nitatoa ajira kwa vijana wenzangu kwa sababu sita weza kufanya kazi peke yangu.
Hata hivyo Joti alifafanua kuwa Chaneli yake itahusika na shughuli zake pekee mtu asitegemee kuona taarifa za habari na mambo mengine kama chanel za watu wengine.
Aidha Joti alisema kuna wachekeshaji wengi chipukizi wanafanya vizuri ila hawataki ushauri, wala hawana mtu waliyempenda ili kuingia katika hiyo kazi hili nitatizo na mtu kuwa staa lazima uwe na historia huwezi kukurupuka na kuwa staa.
“Mimi nimepitia analogi na digital na nimejua vitu vingi kwa kuwa nilipitia kote ninauwezo wa kuutunza ustaa wangu hata miaka 15 ijayo kwa sababu najua kwenda na wakati, tatizo liko kwa vijana wanaochipukia wanataka kuwa Digital tu, pia hawana historia, hawashauriki ndipo tunapowaangalia na kwa sababu najua vurugu zake zote lazima akutane na ukuta na mimi simu yangu iko wazi muda wowote kwa anayetaka ushauri kutoka kwangu.”
Sikufahamu kama ninakipaji ila King Majuto ndio sababu amenipotezea sana muda, na amekula sana hela zangu wakati huo nilikuwa nikiona kuna onyesho lake shuleni basi lazma niingie, pia kumuangalia kwenye tv, lazima nipoteze muda kumuangalia hadi linikuwa nikipigwa sana na wazazi wangu kumbe ni kitu ambacho nilikuwa nakuja kukifanya ndio maana nilikuwa nakifuatilia sana ila bila kujua kama nitakuja kuwa mchekeshaji.
“Napita kwenye ugumu mwingi sana, kwa sababu unaweza ukapita sehemu mtu mmoja akakuomba kupiga picha ukakubali basi wataibuka wengine hapo hata 30 na huwezi kukataa ukikataa hata kama unachelewa utasikia wanasema supa staa Bongo neno ambalo naliogopa sana katika maisha yangu kwani hao wanaosema hivyo ndiyo mashabiki wangu wa wanaweza kunipandisha au kunishusha.’