27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

Joshua akubali kichapo cha TKO

NEW YORK, MAREKANI 

BONDIA wa uzani mzito Andy Ruiz Jr, ameushangaza ulimwengu kwa kumchapa bingwa wa ngumi katika uzani huo Anthony Joshua kwa TKO, usiku wa kuamkia jana. 

Joshua ambaye amekuwa akipewa sifa kubwa za kuja kumrithi bingwa wa zamani katika uzani huo Mohamed Ali, aliangushwa mara nne kabla ya refa kuingilia kati na kusitisha pigano hilo wakati wa raundi ya saba.

Andy Ruiz Jr aliushangaza ulimwengu katika historia ya ndondi na kufanikiwa kushinda mataji hayo matatu IBF, WBO na WBA yaliokuwa yakimilikwa na Anthony Joshua. 

Katika pigano lililovutia wengi kwenye ukumbi maarufu wa ngumi jijini New York, nchini Marekani, New York Madison Square Garden, Ruiz alionekana yupo vizuri zaidi ya Joshua toka awali kwa kumzidi nguvu na maarifa. 

Joshua alipewa nafasi kubwa ya kushinda pambano hilo, lakini mambo yakawa tofauti na watu wakafananisha kilichompata bondia huyo sawa na waliyoyapitia mabingwa wa zamani Lennox Lewis na Mike Tyson ambao pia waliwahi kupigwa na wapinzani ambao hawakupewa nafasi kubwa, lakini waliweza kushangaza ulimwengu wa masumbwi.

Tyson alitandikwa na James ‘Buster’ Douglas mwaka 1990 wakati huo Lewis alichapwa na Hasim Rahman mwaka 2001. Hata hivyo promota wa Joshua, Eddie Hearn, ameweka wazi kuwa bingwa huyo atakuja kulipa kisasi mwishoni mwa mwaka huu.

Hata hivyo Ruiz alionyesha uwezo mkubwa katika pigano hilo ikimaanisha kwamba Joshua atakuwa na kazi ya ziada kumshinda katika pigano hilo linalosubiriwa kwa hamu huko jijini London.

“Joshua alikuwa ameshindwa katika raundi mbili, lakini alishinda moja, ninaamini atapata fursa ya kujirekebisha katika mechi ya marudio jijini London kabla ya Disemba mwaka huu.

“Kwa sasa mazungumzo yoyote ya kuzipiga dhidi ya Tyson Furry au Deontay Wilder yamesitishwa,” alisema Promota huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles