23.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

Jonesia, Linah wameiwakilisha vyema Tanzania AFCON

JESSCA NANGAWE-DAR ES SALAAMFAINALI za Kombe la Mataifa ya Afrika  (Afcon) kwa upande wa wanawake, imehitimishwa juzi huko nchini Ghana,  huku Watanzania wawili, Jonesia Rukya pamoja na Linah Kessy wakiula baada ya kupewa jukumu la kusimamia michuano hiyo mikubwa Afrika.

Mchezo huo wa fainali ulizikutanisha timu za Nigeria na Afrika Kusini, ambao ulichezeshwa na mwamuzi kutoka Zambia.

Wakati Linah akiteuliwa kuwa kamishna wa mchezo wa fainali hizo zilizomalizika Jumamosi iliyopita, mwenzake Jenosia Jonesia naye alikua miongoni mwa waamuzi 13 walioteuliwa kuchezesha michuano hiyo mwaka huu.

Michuano hiyo iliyofanyika kwa wiki mbili mfululizo ilianza kutimua vumbi Novemba 19 nchini humo.

Jonesea ni miongoni mwa waamuzi 13, wa kati walioteuliwa kuchezesha mechi hizo pamoja na wasaidizi 12, kutoka katika mataifa mbalimbali barani Afrika.

Kwa uteuzi huo, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia alimpigia simu Jonesia kumpongeza kwa hatua hiyo ambayo ni sehemu kubwa ya mafanikio ya soka la Tanzania kufanya vema katika medani za kimataifa.

Kuteuliwa kwa wanawake hao kumezidi kuonyesha upeo wa soka la Tanzania lilipofikia sambamba na uwezo wao wanapokua kazini, kwani tayari wamejitengenezea heshima kubwa kwa taifa na hata kimataifa kutokana na kuaminiwa kwao.

Hii inazidi kutoa picha ya jinsi soka la wanawake hapa nchini linavyozidi kupiga hatua na kupewa heshima yake kwa wasimamizi wake kuendelea kuaminiwa kila wakati.

Hii si mara ya kwanza kwa Jonesia kupewa majukumu makubwa kama haya, kwani tayari alishachezesha mashindano mbalimbali, yanayosimamiwa na Shirikisho la Soka barani Afrika (Caf)  na tayari amejitengenezea heshima kubwa.

Mbali ya kupewa majukumu mazito kama hayo, pia mwamuzi huyo amekua akipewa nafasi ya kuchezesha mechi kubwa za Ligi Kuu Tanzania Bara, hasa zile zinazokutanisha mahasimu wakubwa Simba na Yanga.

Pia mwamuzi huyo mwenye beji ya FIFA, aliwahi kuteuliwa kuungana na waamuzi kutoka nchini Kenya, kuchezesha mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake wenye umri chini ya miaka 17 (WWC-Q 17) mwishoni mwa mwaka jana.

Tukirudi kwenye michuano ya (Afcon) ilianza kutimua vumbi, Novemba 17 na kuhitimishwa Desemba1, pia imeendelea kuwapa sifa ya kipekee wanawake hawa kwani wamejiongezea heshima katika kazi zao na kuzidi kuaminiwa.

Michuano hiyo itatumika kutoa timu zitakazofuzu kushiriki kombe la Dunia la FIFA kwa wanawake mwakani nchini Ufaransa, ambapo timu tatu za juu baada ya (AFCON) kuisha ndio zitakazokuwa zimefuzu.

Katika mchezo wa fainali namba 16 uliochezwa katika uwanja wa Accra Sports mjini Accra Saa 10:00 jioni, ulichezeshwa na mwamuzi kutoka Zambia Glady Lengwe aliyesaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja kutoka Madagascar Lidwine Rakotozafinoro, mwamuzi msaidizi namba mbili Bernadettar Kwimbira kutoka Malawi na mwamuzi wa akiba Fatou Thioune.

Nchi  zilizoshiriki katika michuano hiyo ni pamoja na Algeria, Burkinafaso, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati,Congo, Ethiopia, Gambia, Nigeria,Morroco,Uganda, Zambia, Zimbabwe,Afrika Kusini, Senegal, Mali, Libya,Kenya, Lesotho, Ivory Coast, Eswatin, Equatorial Guinea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,184FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles