Quebec, Canada
Kutoka Quebec nchini Canada, mwimbaji nyota wa Injili, Jonathan Budju, ametamba kukata kiu ya wapenzi wa muziki huo baada ya kuachia video ya wimbo, Only You God.
Budju a.k.a Son of God, amesema tangu alipotoa audio ya wimbo huo, mashabiki kutoka kila pembe ya Dunia walikuwa na shauku ya kuona video hivyo anaamini amekata kiu ya wafuasi wake.
“Video tayari imetoka ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube, kama ambavyo mashabiki walinipa sapoti nilipotoa audio naamini hata video ya Only You God itafanya vizuri kwa sababu ina ujumbe mzuri na video ni kali sana hivyo naomba sapoti kwako,” amesema mwimbaji huyo mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.