26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Jokate, wasanii wampa pole Meneja wa Diamond aliyepata virusi vya corona

Anna Potinus, Dar es Salaam

Baadhi ya wasanii na watu mashuhuri wamejitokeza kumpa pole Meneja wa msanii wa muziki, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sallam SK ambaye amethibitisha kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram leo Alhamisi Machi 19, Sallam ameweka ujumbe unaosema kuwa baada ya kufanyiwa vipimo alipata majibu yaliyoonesha kuwa ana maambukizi ya virusi hivyo na sasa yupo chini ua uangalizi maalumu kwa ajili ya kupatiwa matibabu.


“Ninaishukuru serikali kwa maandalizi mazuri na huduma ninayopata wodini kwenye kituo toka juzi niko peke yangu kama nimekikodisha vile, wahudumu wana ushirikiano mzuri Mungu awalinde na awape afya njema maana wamejitolea nafasi zao kutupatia huduma sisi waathirika.


“Hili janga la kimataifa linakwepeka kama tutafuata ushauri nasaha kutoka kwenye wizara husika, ninaomba wote tuwe salama na familia zetu tuchukue tahadhari mapema,” amesema Sallam.


Baadhi ya waliompa pole ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, msanii Ambwene Yesaya ‘AY’, Rita Paulsen, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Hamisi Taletale ‘babutale’, Mbwana Yusuph ‘Mbosso’ na wengine wengi.


Kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, hadi sasa wagonjwa wa corona nchini wamefikia watano.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,608FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles