29.7 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

JOKATE: NITAZUNGUMZIA KUTENGULIWA KWANGU NIKIWA TAYARI

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kaimu Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Jokate Mwegelo atazungumzia suala la kutenguliwa kwa uteuzi wake wa nafasi hiyo wakati akiwa tayari.

Uamuzi wa kutenguliwa kwa uteuzi huo wa Jokate, ulitangazwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James mjini Dodoma jana Jumapili Machi 25, na kuongeza kuwa nafasi hiyo itajazwa baadaye.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Jumatatu, Machi 26 Jokate amesema: “Siko tayari kuzungumzia suala hilo kwa sasa, nitazungumza nikiwa tayari, wakati ukifika nitasema.” Hata hivyo, Jokate hakusema ni lini atakuwa tayari kuzungumzia suala hilo.

Katibu Mkuu wa Shaka Hamdu Shaka uamuzi wa kutenguliwa kwa uteuzi wa Jokate ni maazimio ya Baraza Kuu la Jumuiya hiyo ambapo kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM iliyokutana kwa dharura jana mchana chini ya Mwenyekiti wake Kheri iliazimia hatua hiyo.

Jokate ametumikia nafasi hiyo kwa miezi 11 tangu ateuliwe Aprili 24, mwaka jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles