29.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Jokate mgeni rasmi Jukwaa la Wanawake

Na Beatrice Kaza, Mtanzania Digital

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, Jokate Mwegelo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Jukwaa la Wanawake lililoandaliwa na Irada Style ambalo linalenga kumsaidia mwanamke kutimiza malengo yake kupitia mavazi na muonekano wake.

Mmiliki wa Irada Style, Irada Mahadhi.

Lengo la kukutana kwa pamoja wanawake hao wabunifu ni kuendelea kusherehekea siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 8 Machi, kwa kuonyesha bunifu zao mbalimbali ikiwemo kufanya mnada wa nguo ambapo fedha zitakazopatikana kupitia mnada huo zitaenda kusaidia vituo vya watoto yatima na wale wasiojiweza katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam mapema Machi 13, 2023 Muanzilishi na mmiliki wa Irada Style, Irada Mahadhi amesema Jukwaa hilo litafanyika Machi 17 saa 12 jioni hadi saa 4 usiku katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam ambapo kutakuwa na uzinduzi wa fashion shoo ya Ramadhan na Eid Collection ambayo hufanyika kila mwaka.

“Wakati tunaanzisha Irada Style lengo letu kuu likikuwa ni kuwasaidia mabinti wote ambao wanapenda kuonekana wamependeza katika mavazi yakistaarabu.

“Tutazindua fashion shoo ya Ramadhan na Eid Collection ambapo tutawachagua hawa wanawake ambao tumeweza kuwapa ujuzi katika muda wa mwaka mzima kutimiza malengo yao ya kibiashara hususani kuwapa fursa tofauti tofauti ikiwemo katika upande wa ubunifu wa mavazi na mitindo,” amesema Irada.

Irada amesema jukwaa hilo litahudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka serikalini na taasisi tofauti tofauti lakini pia wafanyabiashara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles