26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Jokate ahimiza jamii kutembelea wagonjwa

 AVELINE KITOMARY – DAR ES SALAAM 

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo ameihimza jamii kuendelea kuwa na utaratibu wa kutembelea wagonjwa hospitali ili kuwafariji.

Joketi aliyasema hayo mwishoni mwa wiki Dar es Salaam, wakati akipokea msaada wa vifaa tiba vilivyotolewa na Jema Foundation kwa ajili ya wagonjwa wanaopatiwa matibabu ya saratani Taasisi ya Saratani Ocean Road.

Taasisi hiyo, inasimamiwa na Jema Baruani ambaye ni miongoni mwa wagonjwa waliowahi kutibiwa saratani Ocean Road na kupona, sasa amejitolea kuendelea kuelimisha jamii kuhusu magonjwa hayo.

“Nahimiza jamii kuendeleza utamaduni wa kuwatembelea, kuwajulia hali wagonjwa waliolazwa wodini, hospitalini walimolazwa ili kupatiwa matibabu dhidi ya maradhi mbalimbali yanayowakabili.kwasababu hakuna anayeijua kesho yake,” alisisitiza.

Aliwapongeza Jema Foundation kwa kujitoa kwa jamii hususan wagonjwa wa saratani kwa kuwatembelea na kuwafariji kila mwaka.

“Nawapongeza madaktari na wataalamu wote wa Ocean Road kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuwahudumia wagonjwa hawa,” alisema.

 Aliongeza “Kipekee naipongeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imesimika vifaa vya kisasa hapa Ocean Road,sasa tunashuhudia inapokea wagonjwa wengine pia kutoka nje ya Tanzania.

“Daktari (Crispin Kahesa), amenieleza wanapokea wagonjwa kutoka nje ya nchi kwa sababu kuna uwezekaji mkubwa umefanywa na Serikali kwa kusimika mashine ambazo wenzetu kwenye nchi zao hawana.

“Amenieleza, huduma za tiba ya saratani zinayopatikana Tanzania ni bora za viwango vya kimataifa na gharama ni nafuu kulinganisha na mataifa mengine.

“Haya ni mambo ambayo lazima tuwaambie Watanzania, wajue kwamba tuna vitu ambavyo wengine wanatamani kuwa navyo, waje wapatiwe huduma bora,” alitoa rai. Mwakilishi wa Jema Foundation, Baruani alisema wagonjwa wengi wa saratani huwa na hofu pale wanapogundulika, wapo wengine ambao huacha matibabu.

“Si wote huwa na moyo wa ujasiri kama mimi, wapo wanaokata tamaa, si wote wana uwezo wa kulikabili gonjwa hili, inabidi sisi ambao Mungu ametujalia, tujitoe katika hali na mali, kuwaona… unaweza ukaja hapa japo kuwaambia neno pole, ikawa ahueni kwao,” alisema.

Mkurugenzi wa Kinga wa ORCI na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani, Crispin Kahesa alisema kila mwaka inakadiriwa Tanzania kuna wagonjwa wa saratani zaidi ya 42,060 asilimia 13 ndiyo hufika hospitali ni takriban wagonjwa 12,600.

“Hawa  wanaokuja hospitalini asilimia 70 ndiyo huweza kukaa na kuendelea na tiba, asilimia 30 huwa wanakatiza au wanapotea kwa sababu tofauti tofauti ikiwamo mtazamo na hofu waliyonayo juu ya ugonjwa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles