27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

John Nini kuwapa raha mashabiki kwa ‘Iza Bella’

COPENHAGEN, DENMARK

BAADA ya kimya cha muda mrefu msanii wa kizazi kipya kutoka Denmark, John Nini (Neza Music), Ijumaa hii amerudi kivingine na wimbo, Iza Bella.

Akizungumza na MTANZANIA DIGITAL, John Nini mwenye asili ya Burundi amesema Julai mwaka huu alirudi nchini kwake ikiwa ni miaka 25 imepita na kukutana na ndugu jamaa na marafiki huku jambo kubwa ni kufanya wimbo huo ambayo unapatikana kwenye mitandao yote ya kuuza na kusikiliza muziki duniani.

“Nimetengeneza wimbo wa kirundi na video pia imetengenezwa nchini Burundi. IZA BELLA ndio jina la ngoma na kuanzia sasa unaweza kuisikiliza audio kwenye Spotify, iTunes, Google Play, Amazon Music na Tidal na video ya muziki itapatikana kwenye chaneli yangu ya YouTube Ijumaa ya Agosti 13.

“Tayari ninaweza kukuambia kuwa wimbo huu Iza Bella ni maalumu msimu huu wa kiangazi na majira ya joto na nina amini utapendwa na waafrika wengi kote duniani hasa wale wanaopenda muziki wa Afro Trap Music,” amesema mwanamuziki huyo ambaye unaweza kumfahamu vizuri kupitia www.johnnini.com.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,409FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles