NYOTA wa muziki wa rap nchini, John Saimon ‘Joh Makini’, amesema vifaa duni vya waongozaji video nchini ndivyo vinavyosababisha wasanii wengi wakimbilie kwa waongozaji wa video wa Afrika Kusini.
Akizungumzia video yake ya ‘Don’t Bother’ ambayo imemgharimu takribani milioni 32, Joh Makini alisema kuwa waongozaji wa nje wana vifaa vya kisasa ambavyo vinafanya video ziwe na ubora wa kimataifa.
“Mimi naamini tunaweza kufanya video zetu hapa nchini kama waongozaji wetu wataboresha vitendea kazi vyao ikiwemo kamera ili video ziwe na kiwango cha kimataifa, zichezwe kwenye vyombo vikubwa,” alisema Joh Makini.
Aliongeza kuwa video hiyo aliyofanya mtayarishaji Justine Campos itakuwa ni wimbo wa mwisho kwa mwaka huu kwake.
Hata hivyo, John Makini, anatakiwa afahamu kwamba wapo waongozaji wazalendo wenye vipaji na uwezo mkubwa wa kufanya video hizo wanazotaka kama watawapa bajeti kubwa katika kazi zao hizo akiwemo Adam Juma, Hanscana, Pablo na wengine wengi.