24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

JMAT kufanya kazi Kimataifa

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) imeingia makubaliano ya kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya amani duniani ili kusimamia utunzaji wa amani duniani.

Makubaliano hayo yaliingiwa wakati wa mkutano wa amani duniani uliofanyika Agosti 17 hadi 19, 2023 Korea ya Kusini ambapo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mariadhiano na Amani Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum alihudhuria.

Mratibu wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania, Fatma Kikkides, akizungumza kuhusu kuteuliwa kuwa Balozi wa Shirika la Kimataifa linalojihusisha na masuala ya amani ya wanawake.

Akizungumza Oktoba 12, 2023 Katibu wa jumuiya hiyo, Israel Maasa, amesema ushiriki katika mkutano huo na ziara nyingine zilizofanywa na mwenyekiti huyo nchini Kenya na Iran zimekuwa na mafanikio makubwa.

“Jumuiya yetu imezidi kujenga mahusiano na taasisi za kimataifa zinazoshughulikia masuala ya amani, na mratibu wetu Fatma Kikides amepewa ubalozi kupitia Shirika linalojihusisha na masuala ya amani ya wanawake,” amesema Maasa.

Naye Alhad Mussa amesema wataendelea kuisaidia Serikali kuhakikisha utaifa na amani inaendelea kustawi na kudumu kwa kuwa ndio vipaumbele vyao.

“Wenzetu wameshaonja na hawataki kabisa kusikia habari ya vita na uvunjifu wa amani, machafuko, ugomvi, uchochezi kwa sababu ni vitu hatari sana. Tuendelee kusikilizana na kuvumiliana, tusiruhusu hata kidogo uchochezi wa aina yoyote ile, tuiache Tanzania iendelee kuwa kitovu cha amani,” amesema Alhad Mussa.

Mratibu wa JMAT na Balozi wa Shirika la Kimataifa linalojihusisha na masuala ya amani ya wanawake, Fatma Kikkides, amesema amejipanga kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa amani na athari za uvunjifu wa amani ili kuhakikisha kunakuwa na ustawi kwa mataifa yote.

Jumuiya hiyo pia imempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutunukiwa Udaktari wa Heshima na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru (JNU) India na kuwataka Watanzania waendelee kumuunga mkono kwa ustawi wa maendeleo ya taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles