24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

JKTMLALE NI MWAMBA WA KIJESHI

Na  AMON MTEGA, SONGEA


KUTOKANA  na ongezeko la vijana wasomi hapa nchini kuwa kubwa  huku ajira serikalini zikiwa zinasuasua  namna ya upatikanaji  vijana hao wanatakiwa kulipunguza tatizo hilo kwa kujifunza  kozi mbalimbali  zenye fursa za kujiajiri.

Kozi hizo zimekuwa zikipatikana katika  vyuo mbalimbali vya Ufundi Stadi (VETA) na pamoja  kwenye maeneo ya Vikosi vya Jeshi  la Kujenga Taifa (JKT) ambapo hutolewa mafunzo namna ya kutumia vipaji mbalimbali ambavyo vitawawezesha namna ya kujiajiri.

Hali hiyo imejidhihirisha  kwenye kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mlale kilichopo Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma kutokana na kikosi hicho kuibua miradi mbalimbali ambayo hufanywa na vijana wa operesheni Magufuli yanayoambatana na mafunzo ya  ukakamavu na uzalendo kwa Taifa .

Kikosi hicho cha 842KJ Mlale kimeweza kubuni miradi ambayo imekuwa na tija kwa vijana ambao wapo kwenye mafunzo ya awali ya kijeshi ambayo yanakwenda sambamba na uibuaji wa miradi kwa kuitendea kazi kwa vitendo ambavyo vinawasaidia vijana kuwa wabunifu wa kupata ajira.

Akizungumza Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya kikosi hicho pamoja na kufunga mafunzo kwa wahitimu wa miezi sita kwa vijana wa operesheni Magufuli  alisema kuwa  kikosi hicho kimeonesha mfano wa namna ya vijana wenye elimu za kada mbalimbali wanavyoweza kujiajiri.

 

Meja Jenerali Isamuhyo alisema kuwa kama vikosi vyote vya mafunzo ya awali ya kijeshi  vikasimama katika ubunifu wa miradi kama kikosi cha JKT Mlale, vijana wengi waliobahatika kupata mafunzo hayo watakuwa na ujuzi mkubwa wa kujiajiri na kuachana na utegemezi wa ajira za serikalini.

Wakati akikagua miradi iliyoibuliwa na kikosi hicho cha Mlale mkuu huyo wa Jeshi la kujenga Taifa nchini alisema kuwa hakuna namna nyingine ya tatizo la ajira serikalini zaidi ya kupanua wigo wa vitengo husika vya kimafunzo  kutoa elimu ya kuwawezesha vijana namna ya kujiajiri.

“Nimepitishwa kwenye miradi yenu nimeridhika kabisa na utendaji wenu pamoja na hivyo nimefurahishwa na mafunzo ya kizalendo ambayo nimeyaona kwa vijana hawa ambao wametimiza miezi sita kwenye kikosi hiki,”alisema Meja Jenerali Isamuhyo.

Miradi ambayo imeibuliwa kwenye kikosi hicho ni uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha kuchakatia mahindi ambao hadi kukamilika kwake kitagharimu zaidi ya Sh.milioni 250 ambacho kitakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wakazi wa baadhi ya vijiji vinavyozunguka kikosi hicho kwa kuwa baadhi yao watanufaika  kwa kwenda kuuza nafaka zao kwa bei inayofaa.

Hata hivyo miradi mingine ni kilimo cha nyanya, npunga,vitunguu, matango,matikiti ,mboga mboga pamoja na kilimo cha mahindi ambavyo vyote hivyo vimeibuliwa na vinafanywa na vijana waliopo kwenye mafunzo hayo na kinatumia umwagiliaji.

Hata hivyo amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya kijeshi kwenda kuyatumia mafunzo hayo kwa kujiajiri katika sekta mbalimbali ikiwamo katika sekta ya kilimo ambayo hutoa fursa kubwa ya ajira.

Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha JKT Mlale, Luteni Kanali Absolomoni Shausi alisema kuwa wameibua miradi hiyo baada ya kutambua kuwa wamekuwa na fursa mbalimbali za mazao ya nafaka yakiwamo mahindi pamoja na ya mboga mboga.

Aidha Luteni Kanali  Shausi alisema licha ya uibuaji wa miradi hiyo lakini bado baadhi ya vijana wa mafunzo hayo wamekuwa ni mafundi wa fani mbalimbali ikiwamo ujenzi wa majengo .

Alisema kuwa kutokana na fani hizo kikosi hicho kimeweza kufanya shughuli  za tenda za ujenzi wa majengo  ya taasisi mbambali ikiwamo ujenzi wa shule za msingi mbili ya Lusilingo na Yola za Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma ambayo yaligharimu Sh.milioni 242 kwa madarasa 10 na matundu ya vyoo 20.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dk, Oscar Mbyuzi alisema kuwa Halmashauri yake iliamua kutoa tenda hiyo kwenye jeshi hilo ambayo ilikuwa ya Sh.milioni 242 kwa shule zote mbili madarasa 10 na matundu ya vyoo 20 na yamekamilika kwa wakati na kwa gharama nafuu.

Mbyuzi alisema kuwa utoaji wa tenda hiyo kwenye jeshi hilo kunawasaidia vijana ambao wapo kwenye mafunzo kutambua namna ya kuziona fursa za kujiajiri pindi wanapohitimu mafunzo yao hivyo ni vyema hata baadhi ya taasisi hasa za kiserikali zikaona umhimu wa kutumia vikosi vya Jeshi la Kujenga Taifa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles