30.4 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

JKT yastisha mafunzo ya kujitolea kwa mwaka 2020/21

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limesitisha mafunzo ya JKT kundi la kujitolea kwa mwaka 2020-2021.

Hivyo, limewataka vijana  ambao walikuwa bado  hawajaripoti wasiende   kuripoti katika makambi waliyopangiwa mpaka hapo itakapotangazwa tena na wale ambao wamefika kurejea nyumbani.

Hayo yameelezwa jana Januari 19, 2021 na Kaimu Mkuu wa Utawala JKT, Kanali Hassan Mabena wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.

Kanali Mabena amesema mafunzo hayo yalikuwa yaanze hivi karibuni katika makambi mbalimbali nchini hivyo wameyasitisha kwa muda mpaka hapo itakapotangazwa.

Amesema kutokana na kusitishwa kwa mafunzo hayo JKT inawataka vijana wote ambao walichaguliwa na kuripoti makambini kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya JKT  ya kujitolea warejee majumbani kwao.

Kanali Mabena amesema na wale ambao walikuwa bado  hawajaripoti wasiende   kuripoti katika makambi waliyopangiwa mpaka hapo itakapotangazwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles