31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

JKT wapeleka kikosi Kibiti

Grace Shitundu -Pwani

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limezindua kikosi kipya kilichopewa jina 830 KJ   kilichopo kijiji cha Mkupuka Kata Mchukwi wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.

Akizungumza wakati akizindua kikosi hicho, Mkuu wa JKT,  Brigedia Jenerali  Charles Mbuge amesema kikosi cha  830 KJ Kibiti ni eneo la kimkakati la kuhakikishaa ulinzi na usalama pamoja  na kutoa malezi kwa vijana.

Pamoja na hayo Mkuu huyo wa JKT amewaasa wananchi  wa maeneo ya kibiti  kutoingilia mipaka ya eneo la jeshi  sambamba na kuhakikisha wanatoa taarifa zozote zinazohatarisha amani.

“Kuanzishwa kwa kikosi hiki ni faida kubwa kwa wakazi wa maeneo haya, kikosi hiki ni eneo la kimkakati kwa aajili ya ulinzi na usalama, malezi ya vijana wetu, na uzalishaji mali.

” Ninawaomba wananchi tuishi kwa kupendana na kushirikiana, baadhi yetu wanajua kilichotokea na hali ilivyokuwa kipindi cha nyuma,  nawasihi kutoa taarifa pindi kunapokuwa na viashiria vya kutishia usalama na amani” alisema mkuu huyo wa JKT.

Alisema kuanzishwa kwa kikosi hicho ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhakikisha wanakuwa na kikosi maeneo hayo.

Alisema majukumu ya JKT ni  katika uzalishaji  mali, malezi kwa vijana, ulinzi na usalama hivyo hiyo itakuwa ni faida kubwa na wataendelea kutafuta maeneo mengine kuongeza uwezo wa kuwapokea vijana wengi zaidi.

” Nawasihi wananchi kushirikiana nasi lakini wasiingilie mipaka ya eneo la jeshi  kwani pamoja na malezi ya vijana na ujasiliamali pia ulinzi ni wajibu wetu wote”

Kwa upande wake Mkuu tawi la Utawala, Kanali Julius Kadawi alisema kuanzishwa kwa kikosi hicho ni mafanikio makubwa kwa wakazi wa kibiti.

“Haya ni mafanikio makubwa katika masuala ya uzalishaji mali, michezo na burudani, malezi ya vijana na ulinzi kwa maeneo ya kibiti” alisema.

Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Kibiti JKT, Luteni Kanali Mohamed Karua aliwashukuru wananchi kwa kutoa eneo hilo kwa matumizi ya jeshi na kuahidi kishirikiana nao.

Mkazi wa kijiji cha Mkapuku, Amina Yusuf alisema wamefurahishwa na hatua hiyo na sasa wataishi kwa amani.

” Kipindi cha nyuma tuliishi kwa wasiwasi na mashaka lakini sasa tutakuwa naaamani kwa kuwa ulinzi utakuwa imara zaidi”, alisema Amina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles