JKT Tanzania yaanza kuivutia kasi Yanga

0
881

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa JKT Tanzania, Abdallah Mohammed ‘Bares’, amesema kwa sasa wapo katika mikakati mizito kuona ni vipi wanakabiliana na mechi zao zijazo za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezo wao ujao utakuwa dhidi ya Yanga utakaopigwa Novemba 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

JKT Tanzania ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City, katika mchezo wao wa mwisho uliochezwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Bares alisema kwa sasa wanatafuta mchezo mmoja wa kirafiki ili kuangalia baadhi ya makosa yaliyopo kwenye timu yake tayari kukabiliana na Yanga.

“Kwa sasa tunakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Yanga, hivyo hatuwezi kuzubaa zaidi ya kuendelea kupambana na kufanya maandalizi makubwa kabla ya kukutana na Yanga,” alisema.

Alisema anafahamu akikutana na Yanga, mchezo huwa unakuwa na ushindani mkubwa, lakini kwa kuwa wanafahamu mpira ni dakika 90, wataingia na mbinu mpya kuhakikisha wanapata ushindi.

Bares alisema kikosi chake kipo vizuri, kikiwa hakina majeruhi na kwamba kila mchezaji anaonekana kujituma na kufuata kile anachowafundisha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here