26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

JKCI YASAIDIWA MATAULO MAALUMU YA WAGONJWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Mohamed Janabi (mwenye miwani) akipokea msaada wa taulo maalumu za kuwaosha wagonjwa, kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya PharmKonsult Afrika , Dk. Rugola Mtandu

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imekabidhiwa msaada wa taulo maalumu za kuwaogeshea wagonjwa walioko wodini, zenye thamani ya Sh milioni 13.75 kutoka Kampuni ya PharmKonsult Africa.

Akikabidhi msaada huo juzi hospitalini hapo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Dk. Rugola Mtandu, alisema taulo hizo ni za kisasa na zitasaidia kupunguza maambukizi.

“Tumeleta leo (jana) maboksi 50 ambayo ndani yake kila moja lina taulo 50 zenye thamani ya jumla ya Sh milioni 13.75,” alifafanua.

Dk. Mtandu alisema kwa kawaida wagonjwa wanaolazwa wodini muda mrefu, huwa wanaogeshwa (wanaoshwa), wakiwa kitandani, kitendo ambacho huweza kuchukua hadi dakika 30.

Alisema wakati mwingine mgonjwa huweza kupata maambukizi wakati wa kuoshwa iwapo muuguzi anakuwa amejisahau kunawa mikono yake vema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles