NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM
TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imekabidhiwa msaada wa taulo maalumu za kuwaogeshea wagonjwa walioko wodini, zenye thamani ya Sh milioni 13.75 kutoka Kampuni ya PharmKonsult Africa.
Akikabidhi msaada huo juzi hospitalini hapo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Dk. Rugola Mtandu, alisema taulo hizo ni za kisasa na zitasaidia kupunguza maambukizi.
“Tumeleta leo (jana) maboksi 50 ambayo ndani yake kila moja lina taulo 50 zenye thamani ya jumla ya Sh milioni 13.75,” alifafanua.
Dk. Mtandu alisema kwa kawaida wagonjwa wanaolazwa wodini muda mrefu, huwa wanaogeshwa (wanaoshwa), wakiwa kitandani, kitendo ambacho huweza kuchukua hadi dakika 30.
Alisema wakati mwingine mgonjwa huweza kupata maambukizi wakati wa kuoshwa iwapo muuguzi anakuwa amejisahau kunawa mikono yake vema.