23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

JKCI yaokoa maisha ya wagonjwa 3,330

NA VERONICA ROMWALD- DAR ES SALAAM

TAASISI ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), imeokoa maisha ya watu 3,330 waliokuwa wakisumbuliwa na matatizo mbalimbali ya moyo tangu mwaka 2015 hadi sasa.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi, alipozungumza wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo na kuukaribisha mwaka mpya wa 2019.

 “Huwa naulizwa mara nyingi na waandishi wa habari tumeokoa kiasi gani cha fedha za Serikali, ni vizuri lakini kikubwa kwetu tunajivunia kuokoa maisha.

 “Tangu kuanzishwa rasmi kwa taasisi hii mwaka 2015 hadi sasa tunaposherehekea miaka mitatu, tumeokoa maisha ya watu 3,330, ikiwa wangepelekwa nje ya nchi Serikali ingegharamia kila mmoja shilingi milioni 29.

“Kila mwaka wagonjwa kati ya 200 hadi 350 waliokuwa wakipelekwa nje ya nchi, wengi wao walikuwa ni wenye matatizo ya moyo, ingechukua Serikali miaka ipatayo minane kufikia idadi ya wagonjwa tuliowahudumia ndani ya miaka hii mitatu,” alisema.

Pia alisema katika kipindi hicho mgonjwa mwenye umri mdogo waliyefanikiwa kumfanyia upasuaji alikuwa na miaka minne na kwa upande wa watu wazima alikuwa na umri wa miaka 82.

 “Tunavishukuru mno vyombo vya habari, waandishi wamefanya kazi nzuri, wametangaza habari za taasisi yetu, kazi tunayofanya, sasa hivi Watanzania wanajua wakiwa na matatizo ya moyo waende kutibiwa wapi.

 “Nawapongeza pia wafanyakazi wote kwa sababu wameendelea kufanya kazi kwa bidii, ufanisi wao umekuwa chachu ya huduma bora tunazotoa, nawasihi wasichoke, wazidi kuchapa kazi.

 “Ili tunapoanza miaka mitatu mingine kuanzia sasa, tukijaliwa kufika tuendelee kujivunia kuwa taasisi bora na ya mfano wa kuigwa katika utoaji huduma,” alisema.

Pia aliwatunuku vyeti baadhi ya waandishi wa habari akiwamo mwandishi wa habari za masuala ya afya na jamii wa gazeti hili, Veronica Romwald, kutambua mchango wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles