24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

JKCI yafanya upasuaji mwingine wa moyo

Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), wakimfanyia upasuaji wa kupandikiza mashine mbili (Pacemaker CRTD) mwanaume ambaye moyo wake umechoka kufanya kazi ya kusukuma damu, upasuaji huo ulifanyika juzi.
Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), wakimfanyia upasuaji wa kupandikiza mashine mbili (Pacemaker CRTD) mwanaume ambaye moyo wake umechoka kufanya kazi ya kusukuma damu, upasuaji huo ulifanyika juzi.

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

TAASISI ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imefanya upasuaji mwingine wa kihistoria kwa kuweka mashine mbili tofauti katika moyo uliochoka.

Mashine hizo zimewekwa katika moyo wa mwanamume mwenye umri wa miaka 68, ili kuusaidia uweze kufanya kazi sawasawa.

Upasuaji huo umefanywa chini ya madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa JKCI, wakishirikiana na wenzao wa kutoka nchini Kenya.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu jana, Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi alisema upasuaji huo ulifanyika juzi hospitalini hapo.

Hata hivyo Dk. Janabi hakutaka kutaja jina la mgonjwa huyo kutokana na sababu ambazo hazikuweza kufahamika mara moja.

“Huu ni upasuaji wa aina yake na wa kihistoria kufanywa na JKCI, naweza kusema ni zaidi ya kuweka betri kwenye moyo maana ile ni mashine moja, sasa mgonjwa huyu tumemwekea mashine mbili zilizopo katika kifaa kimoja ambacho kitaalamu kinajulikana kama pacemaker CRT-D.

“Mashine moja ni kwa ajili ya kuzalisha umeme wa kushtua moyo wake uweze kufanya kazi iwapo utasimama na mashine nyingine ni kwa ajili ya kusaidia mapigo ya moyo wake kwenda sawasawa jinsi inavyopaswa,” alisema.

Profesa Janabi alisema mgonjwa huyo anaendelea vizuri  na amewekwa kwenye chumba cha mapumziko.

“Leo (jana) siwezi kutaja jina lake gazetini maana ni lazima mwenyewe aridhie jambo hilo, nakusihi kesho (leo) uje tutamwomba azungumze na wewe lakini hajambo kabisa, tumemlaza kwenye chumba cha mapumziko,” alisema.

Akizungumza na MTANZANIA hivi karibuni hospitalini hapo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa JKCI, Peter Kisenge alisema mwanamume huyo anakadiriwa kuwa umri wa miaka 68 na kwamba utendaji kazi wa moyo wake ni chini ya asilimia 20.

“Moyo wake umechoka kufanya kazi, utendaji kazi wake ni chini ya asilimia 20, misuli yake imechoka kabisa na haiwezi tena kufunguka ili kusukuma damu iende kwenye mishipa yake na kuisafirisha mwilini mwake ili na yeye aweze kuishi kama watu wengine,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles