26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

JK kutunukiwa shahada ya heshima OUT leo

JKNA MANENO SELANYIKA, DAR ES SALAAM

RAIS mstaafu, Jakaya Kikwete, anatarajiwa kutunukiwa shahada ya heshima cha uongozi kutoka Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania (OUT) kwenye mahafali ya 30   chuoni hapo leo.

Mbali na Kikwete pia Rais wa awamu ya 15 kutoka Chuo Kikuu cha Korea ya Kusini, Profesa  Chae  – Hong Suh pia atatunukiwa shahada ya heshima kwa mchango wake mkubwa wa kuleta mabadiliko katika nchi za Afrika kwa kutumia teknolojia ya sayansi.

Makamu Mkuu wa Chuo  hicho, Profesa  Elifas Bisanda alisema    Rais Kikwete alipokuwa madarakani aliweza kusuluhisha migogoro mbalimbali  ukiwamo  uliotokea   Kenya baada ya uchaguzi 2007.

“Mkuu wa chuo hiki leo atawatunuku viongozi hao pamoja na wengine ambao jumla watakuwa 69 katika fani mbalimbali,” alisema Bisanda.

Profesa Bisanda alisema Kikwete alipokuwa madarakani aliweza kukuza na kuimarisha uchumi wa Tanzania na kutembelewa na marais wa dunia hivyo ana kila sababu ya kupewa cheti hicho.

Katika mahafali hayo   wahitimu watatu watatunukiwa Shahada ya Pili ya Uzamivu (PHD), wahitimu 20 watatunukiwa Shahada ya Uzamili katika fani za uchumi na elimu na wengine 22 watatunukiwa shahada ya kwanza wakati Stashahada watakuwa 15 na Astashahada watakuwa sita.

Bisanda alisema chuo hicho kimeweza  kufungua matawi kila mkoa lakini na ni chuo pekee nchini chenye wanafunzi wanaosoma nje ya nchi kupitia masafa marefu kwa kutumia Tehama.

Alisema katika mahafali yaliyopita zaidi ya wanafunzi 26 kutoka mataifa mbalimbali walitunukiwa vyeti.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles