23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

JK AWANYOSHEA KIDOLE WAMILIKI WA VIWANDA

Na GUSTAF HAULE-Kibaha

RAIS mstaafu, Jakaya Kikwete, amewataka wamiliki wa viwanda kuacha kuwakandamiza wakulima kwa kununua mananasi yaliyomo shambani kwa bei ya chini.

Kikwete ambaye pia ni mkulima wa zao hilo, alitoa kauli hiyo juzi katika shamba lake lililopo Kiwangwa wilayani Bagamoyo.

Alisema   licha ya viwanda kusaidia kupatikana   masoko ya ndani, vimekuwa havina  uwiano wa gharama zinazolingana na maumivu anayoyapata mkulima.

Alisema wakati mwingine  imekuwapo changamoto ya kushuka   soko    hali inayokuwa ikisababisha wakulima kupata hasara kwa matunda kuoza yakiwa mashambani .

Akitoa taarifa ya shamba lake la mananasi wakati msafara wa  Mwenge wa Uhuru ulipotembelea shamba hilo, Kikwete alisema kilimo  cha matunda kina tija  endapo kitalimwa kisasa na kupata soko la uhakika.

“Wakati utafika watakosa matunda kutokana na gharama yao hailipi, wakulima wa matunda tutashindwa kukubali kuuza kwa bei ya chini ambayo hailipi,” alisema Kikwete.

Alimweleza kiongozi wa mbio hizo, Amour Hamad Amor  kuwa mananasi huvunwa baada ya miezi 18 tangu kupandwa.

“Bei ya mauzo hutegemea wanunuzi na wachuuzi wadogo ambao hununua kwa ukubwa wa nanasi kutoka Sh 400 hadi Sh 800 linapovunwa   shambani,” alisema.

Shamba   la kiongozi huyo lina ukubwa wa ekari 200, kati ya hizo 64 zimelimwa na zipo hatua ya kupaliliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles