27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

JK amteua Makalla kuwa RC

mos-MakalaNa Mwandishi Wetu, Dar

RAIS Jakaya Kikwete, amefanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa wawili wapya na kuwahamisha wengine vituo vya kazi.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, ilisema Rais Kikwete amefanya uteuzi huo kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wakuu wa mikoa ambao wanawania ubunge.

Katika uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Amos Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Jordan Rugimbana kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Aidha Rais Kikwete, amewahamisha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mwantumu Mahiza kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga kuchukua nafasi ya Saidi Magalula aliyehamishiwa Mkoa wa Rukwa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Stella Manyanya anayewania ubunge mkoani Ruvuma.

Rugimbana ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mahiza.

Makalla mbaye ni Naibu Waziri wa Maji aliyekuwa mbunge wa Mvomero, Morogoro, anachukua anafasi iliyoachwa wazi na Leonidas Gama ambaye pia anawania ubunge mkoani Ruvuma.

Uteuzi na uhamisho huo ulianza Septemba 12, mwaka huu na wakuu wapya wa mikoa wataapishwa kesho Ikulu, Dar es Salaam.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles