23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

JK aitaka Afrika kuungana kukabiliana na tabia nchi

Jakaya Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete

Na Mwandishi Maalumu, Equatorial Guinea

RAIS Jakaya Kikwete, amesema nchi za  Afrika hazina budi kuungana na kuchukua hatua za kupunguza madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa kwa pamoja.

Hayo aliyasema juzi mjini Malabo, nchini hapa alipokuwa anafungua mkutano wa wakuu wa nchi 11 zinazounda Kamati ya Mazingira ya nchi za Umoja wa Afrika (CAHOSCC).

“Suala la Tabia Nchi barani Afrika ni changamoto na fursa pia kwani kama tukifanya uamuzi mzuri tunaweza kupata manufaa kutokana na mbinu mbalimbali zilizopo za kupunguza madhara yake,” alisema Rais Kikwete.

Kutokana na hali hiyo alizitaka nchi za Afrika kulichukulia suala la Tabia Nchi kwa umakini mkubwa kwani kwa hali tuliyofikia hivi sasa, hakuna chaguo lingine bali kuangalia njia za kupunguza athari zake.

Nchi wanachama wa Kamati ya Mazingira  ya AU ni pamoja na Tanzania ambayo ndiyo Mwenyekiti, Algeria, Ethiopia, Congo-Brazaville, Kenya, Mauritania, Mauritius, Msumbiji na Uganda.

Katika hatua nyingine kamati ya AU imesisistiza kuwa nchi za Afrika zinahitaji kuboresha uwezo wake wa kupata taarifa za tahadhari katika ngazi zote, uwezo wa kifedha, mawasiliano na usafirishaji katika miji yake.

Rais Kikwete yuko Malabo, anahudhuria kikao cha siku mbili cha wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU) kinachoanza Juni 26, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles