27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Jitokezeni kwa wingi kuhesabiwa Agosti 23- Kuhani Mwakibinga

Na Derick Milton, Bariadi

Kiongozi wa Kanisa la World Miracle Mission Central (WMCC) kutoka mkoani Shinyanga, Kuhani Ayubu Mwakibinga amewataka waumini wa kanisa hilo kujitokeza kwa wingi katika zoezi la Sensa ya Watu na Mkazi.

Amesema kuwa zoezi hilo ambalo litafanyika Agosti 23, 2022 ni muhimu sana kwa nchi ambayo inataka kuwaletea watu wake maendeleo, ambapo ameeleza yeye atakuwa mstari wa mbele siku hiyo kuhesabiwa.

Kiongozi huyo wa dini amesema hayo Julai 11, 2022 katika mkutano wake wa injili uliofanyika mjini Bariadi mkoani Simiyu na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi wa mji wa Bariadi wakiwemo waumini wake.

Amesema kuwa zoezi la sensa linatakiwa kuungwa mkono na kila Mtanzania mpenda maendeleo, kwani serikali haiwezi kuleta miundombinu mbalimbali kwa wananchi bila ya kujua wako wangapi na wanahitaji nini.

Ameongeza kuwa watu wengi wamekuwa wakilalamikia Serikali kwa kushindwa kuwaletea huduma mbalimbali za kijamii, ambapo ameeleza ili serikali iweze kutimiza jukumu hilo lazima ijue ina watu wanagapi.

Amewataka wahumini wake kila mmoja kuhakikisha anamwasisha mwezake kwenda kuhesabiwa Agosti 23, 2022, ili serikali iweze kuweka mipango yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.

“Agosti 23, 2022 ni siku ya sensa kitaifa na sisi kama raia wa nchi hii, ambayo inaoongozwa na Mama yetu mpendwa Rais Samia Suluhu Hassan tunao wajibu wa kumuunga mkono kwa kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuhesabiwa, mimi nitakuwa mstari wa mbele kuhesabiwa.

“Nchi lazima iwe na takwimu, tukipanga maendeleao tujue wako wangapi, tunaweka pale kulingana na takwimu za watu walioko pale, tusipohesabiwa tutajua watu wako wangapi?,” amesema Kuhani Mwakibinga.

Katika hatua nyingine Kuhani Mwakibinga amewataka waumini wake kuendelea kumwombea Rais Samia kwani amekuwa kiongozi mwenye maono wa kuletea maendeleo kwa kasi wananchi wake.

“Tumemwona Rais wetu kwa kipindi hiki kifupi amejenga shule, vituo vya Afya kwa wingi sana, tunao wajibu wa kumlinda kiongozi wetu kwa kumwombea na wale wenye nia mbaya na yeye,” amesema Kuhani Mwakibinga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles