32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Jinsi ya kutunza kuku wanaokua kuanzia wiki 8-18

UFAGAJI WA KUKU

Na ZAHOR A. ZAHOR

UTUNZAJI wa kundi hili unategemea mfumo unaotumika.

Kuku wanaofugwa katika mfumo huria.

Kuku wanaofugwa katika mfumo huu wapatiwe matunzo bora

yakiwamo yafuatayo;

  • Wapewe chakula cha ziada asubuhi kabla ya kutoka na wanaporudi kwenye banda. Chakula hicho kinaweza kugawanywa mara ya mbili kwa siku.
  • Wapatiwe maji safi na ya kutosha wakati wote
  • Wapatiwe chanjo na dawa kulingana na ushauri wa mtaalamu wa mifugo. Wiki ya kumi warudie chanjo ya mdondo, wiki ya 12 kuhara (fowl cholera), wiki ya 14 ndui ya kuku.

Kuku wanaofugwa katika mfumo shadidi

  • Majogoo watenganishwe na mitetea katika wiki saba hadi 10 ili kuzuia uzaliano usio na mpangilio.
  • Wapewe chakula cha kukuzia kuanzia wiki ya 8-15 gramu 55-60 na kuanzia wiki ya 16 gramu 65-80 kwa wanaofugwa mfumo huria na gram 120-125 kwa kuku kwa siku kwa wanaofugwa mfumo wa shadidi.
  • Kuku wa nyama wapatiwe chakula cha kuku wa nyama muda wote.
  • Wapatiwe maji safi ya kunywa kwa muda wote kwenye vyombo safi.
  • Kuku wachunguzwe dalili zozote za ugonjwa ili waweze kupata tiba sahihi kutoka kwa mtalaamu wa mifugo.
  • Kuku wa wiki 9-20 wanahitaji nafasi ya mita za mraba 0.15 kwa kuku na wiki 21 au zaidi mita za mraba 0.2.
  • Vyombo maalumu kwa ajili ya chakula na maji.
  • Wafanyiwe usafi wa banda mara kwa mara ili kuzuia magonjwa yanayotokana na uchafu.
  • Wakatwe midomo ili kuzuia kudonoana.

Kuku wanaotaga

Mahitaji ya kuku wanaotaga ni tofauti na makundi mengine.

Mambo ya kuzingatia kwa kuku wanaotaga ni pamoja na:

  • Banda liwe na viota vya kutagia (kiota kimoja kwa kuku watatu hadi watano). Viota viwekwe bandani mara kuku watakapofikisha umri wa wiki 18 ili waanze kuzoea kuvitumia.
  • Wapatiwe chakula na maji safi wakati wote kwa kutumia vyombo maalumu ambavyo ni visafi.
  • Kuku wasiotaga waondolewe kwenye kundi. Kuku hao huonekana wasafi na sehemu ya kutolea yai huwa ndogo na kavu, upanga wake kichwa (comb) huwa mdogo na mwekundu.
  • Wapatiwe dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu.
  • Wawekewe fito au ubao mwembamba kama sehemu ya kupumzikia na mazoezi ili kuzuia kudonoana.
  • Mayai yakusanywe mara 4 au zaidi kwa siku ili yasidonolewe na kuku,
  • Kuwe na malalo makavu na yabadilishwe mara yanapochafuka.
  • Vyombo vifanyiwe usafi ili kuzuia magonjwa.
  • Watundikiwe majani ya mchicha, papai, alfaafa, majani jamii ya mikunde ili kuboresha lishe.

Udhibiti na tiba dhidi ya magonjwa ya kuku

Kuku wanaopata lishe bora, kutunzwa vizuri na kupatiwa chanjo dhidi ya magonjwa huwa na afya nzuri.

Iwapo ugonjwa utatokea, wagonjwa watenganishwe na wazima na wapatiwe tiba.

Kanuni kuzuia

  • Banda liwe safi muda wote.
  • Kabla ya kuweka kuku, banda linyunyuziwe dawa.
  • Kuku wakaguliwe kila siku ili kubaini wagonjwa au wenye

matatizo, kuwatenga na kutoa taarifa kwa mtaalam wa mifugo.

  • Wapatiwe chanjo.
  • Watu wasiohusika wasiingie eneo la kufugia kuku bila utaratibu.
  • Ndege na wanyama wengine wasifike eneo la kufugia.
  • Banda la kufugia kuku litenganishwe na mabanda ya mifugo mingine.
  • Lango la kuingia katika banda la kuku liwekewe dawa ya kukanyaga kwa wanaoingia ndani ili kuzuia kuingiza vimelea vya wadudu.
  • Vifaa vya chakula na maji viwe safi wakati wote.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles