28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

JINSI YA KUPATA MTOTO UNAYEMUHITAJI

Na MWANDISHI WETU,

KATIKA urutubishaji, yai la mwanamke huwa linabeba chromosome X yaani XX na mbegu ya mwanamume hubeba chromosome XY.

Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na Y kutoka kwa mwanamume mtoto wa kiume hupatikana.

Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na X kutoka kwa mwanamume mtoto wa kike hupatikana

Sifa za Chromosomes X na Y za mwanaume

Ili uweze kufanikiwa kuchagua mtoto wa kiume au wa kike lazima ujue sifa za chromosomes zinazoamua jinsia ya mtoto

Sifa za Chromosomes Y

  1. Zina spidi  kubwa kwahiyo kama yai lipo tayari zenyewe  zitawahi kwenda kurutubisha
  2. Zina maisha mafupi kulinganisha na X

Sifa za Chromosomes X

  1. Zina spidi ndogo
  2. Zina maisha marefu kulinganisha na Y.

Baada ya kujua sifa za chromosome ambazo ndio zinatusaidia kuamua jinsia twende moja kwa moja kwenye jinsi ya kupata mtoto wa jinsia unayotaka.

 Mambo ya kuzingatia

  1. Lazima mwanamke ajue mzunguko wake (menstrual cycle) siku ya 1-28
  2. Lazima mzunguko wake uwe na mpangilio sahihi (anaweza kuchunguza mzunguko wake kwa miezi minne mfululizo).
  3. PH ya uke lazima iwe kiwango sahihi 4-5.5 (Muhimu kutumia neplily pad kwa kuwa na PH sahihi.
  4. Ushirikiano kati ya mwanamke na mwanamume ni muhimu pia.

Jinsi ya kupata mtoto wa kiume

Ili uweze kupata mtoto wa kiume kisayansi unashauriwa kushiriki tendo la ndoa siku ambayo yai litakuwa limetoka kama mzunguko wako uko sahihi ni siku ya 14.

Njia nyingine ya kujua yai limetoka baba anapaswa kuingiza vidole viwili ukeni wakati wa asubuhi na akikuta uteute ujue yai limetoka kwahiyo jioni mnapaswa kushiriki tendo la ndoa ili kupata mtoto wa kiume.

Sababu ya kushiriki tendo la ndoa wakati yai limetoka ili kupata mtoto wa kiume

 Kisayansi chromosome Y ambayo inahusika katika kutunga mimba ya mtoto wa kiume ni nyepesi na ina spidi kubwa haiwezi kiishi muda mrefu kwahiyo ukishiriki tendo la ndoa wakati yai limetoka maana yake unaongeza nafasi ya kupata mtoto wa kiume.

Mtoto wa kike 

Ili ufanikiwe kupata mtoto wa kike unatakiwa ushiriki tendo la ndoa siku tatu kabla ya yai kupevuka yaani hapa ni baada ya kujua mzunguko.

 Sababu ya kushiriki siku tatu kabla

Sababu kubwa ni kwamba chromosome X ambazo ndio zinaunda mtoto wa kike huwa zina sifa ya kuwa na maisha marefu na kutembea taratibu hivyo yai likitolewa litakuta chromosome X ziko hai

Baadhi ya wazee wa zamani wanaamini haya katika kupata mtoto wa jinsia unayotaka.

Wanasema ili kupata wa kike unapaswa kula samaki, mboga za majani, matunda, bidhaa za maziwa, mbegu za matikiti maji na alizeti.

Pia wanashauri wakati wa kufanya tendo la ndoa mwanamke akae juu.

Ili kupata wa kiume wanashauri kula nyama, ndizi, vyakula vya chumvi kama chips ila isizidi chumvi, karanga na vyakula vingine vya potassium na sodium.

Chromosomes Y zinahitaji pH ya alkane kuliko asidi ndio maana wazee waliona hili.

Mwandishi wa makala haya anapatikana kwa namba +255 657 910 428/+255 753 937 759

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles