28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Jinsi ya kufanyia kazi nyumbani wakati wa mlipuko wa corona

Leah Mushi, Dar es Salaam

Kwa baadhi ya Mashirika ya Kimataifa kama Umoja wa Mataifa (UN) na Internews kufanyia kazi nyumbani ni moja ya sera ambayo mfanyakazi anaweza kuitumia wakati wowote.

Kufanyia kazi nyumbani haimaanishi usiende kutembea na kufanya shughuli zako, la hasha bali hautakuwa katika jengo la ofisi tu lakini shughuli nyingine ikiwamo kujibu emails na kuhudhuria mikutano kwa njia ya mtandao na shughuli zako zote zinapaswa kuendelea kama kawaida.

Kwa wengi hapa nchini kufanyia kazi nyumbani ni jambo jipya na kwa mara ya kwanza kutokana na janga la homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona.

Wafanyakazi wengi nchi mbalimbali duniani ambao kazi zao zinaruhusu kutokuwepo mahala pa kazi wanajikuta wanapaswa kufanyia kazi nyumbani ikiwa ni namna moja wako ya kujikinga na kusambaza ugonjwa huu ambao hadi sasa hauna tiba wala chanjo.

Kwa hapa nchini bado ugonjwa huo haujaenea sana kiasi cha kuhitajika kufanyia kazi nyumbani lakini ni vema kujiandaa kisaikolojia endapo itatokea umuhimu wa kufanya hivyo kama tahadhari.

JE, UMEJIANDAAJE?

Kupitia makala hii fupi iliyoandikwa na Katie Morell kupitia jarida la American Express unaweza kupata dondoo muhimu za kukuwezesha kufanyia kazi nyumbani kwa ufanisi.

Kwa kifupi dondoo hizo ni pamoja na kujiandaa kisaikolojia kuwa utakuwa mpweke kulinganisha na vile ambavyo umekuwa ukishirikiana na kuwasiliana na wenzako kazini.

Umuhimu wa kuweka muda maalumu wa kufanya kazi na vile vile kufanya shughuli za nyumbani.

Nidhamu ya kupokea simu binafsi na kutazama mitandao ya kijamii.

Nguo uvaazo wakati unafanya kazi zinaweza kukupa hisia ya kuwa upo kazini au la.

Lakini pamoja na yote hayo ni muhimu kupanga mambo yako vema na uwe na muda wa kupumzika na kuacha kufanya kazi pale muda wa kazi ukiisha funga computer yako mpaka kesho yake na upumzike.

Mwandishi wa makala haya Leah Mushi ni Mkufunzi Mwandamizi katika masuala ya Kidijitali.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles