29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

Jinsi ya kuandaa Pizza ya kuku

Mahitaji

  1. Unga wa ngano vikombe 2
  2. Hamira vijiko vya chai 2
  3. Baking powder kijiko cha chai 1
  4. Mafuta ya kula vijiko vikubwa 2
  5. Vitunguu saumu vya unga kijiko kidogo 1
  6. Vitunguu maji vya unga kijiko kidogo 1
  7. Chumvi kijiko kidogo 1
  8. Sukari kijiko kidogo 1
  9. Maji ya vuguvugu kikombe 1

Jinsi ya kuandaa

Changanya vitu vyote na ukande unga wako hadi uwe mlaini vizuri. Baada ya hapo funika na acha uumuke kwa muda wa dakika kama 45 hivi.

Maandalizi ya saurce
Chukua nyanya kubwa sita hadi nane zilizoiva vizuri, kutegemea na ukubwa.
Kitunguu maji kimoja cha ukubwa wa  kati. Vitunguu saumu punje 10.
Giligilani robo kikombe.
Binzari nyembamba kijiko kimoja kidogo.
Maji kikombe kimoja.


Saga vyote kwa pamoja kwenye blenda halafu upike huo mchanganyiko hadi uive. Yaani uwe mzito wa kujaza kikombe kimoja na nusu.

Baada ya hapo, chemsha kuku na utoe mifupa halafu ukate nyama vipande vidogodogo. Kiasi cha vikombe viwili,
cheese vikombe viwili.
Saurce kikombe kimoja na nusu
Spinach kikombe kimoja

Jinsi ya kutengeneza pizza
Chukua unga wako ulioumuka na utengeneze duara kwa kutumia mkono. Usisukume kama chapatti, baada ya hapo
mwagia saurce na uisambaze vizuri.
Weka kikombe kimoja cha cheese
Weka kuku na spinach
Malizia kikombe kimoja cha cheese
Weka kwenye oven kwa nyuzi joto 125 kwa muda wa dakika 20 hadi 25.
Itoe, kisha iache ipoe halafu kata na ufaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles