30.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

JINSI YA KUANDAA MATUNDA MCHANGANYIKO

Fruit-cancerMAHITAJI.

1:PAPAI

2:TIKITI MAJI

3:NANASI

4:EMBE DODO

5:TUFAA (apple)

6:NDIZI ZA KUIVA

7:PARACHICHI

8: STRAWBERIES

9:STAFELI

10:TOPETOPE

 

JINSI YA KUANDAA.

Chukua chombo unachoona kinafaa kwa ajili ya kuweka matunda yako kisha yakatekate vipande vidogo vidogo ili yaweze kulika kwa urahisi na utaandaa kulingana na kiasi cha matunda ulichonacho.

Mara baada ya kuyakatakata yachanganye sawasawa ili yaweze kutoa rojo, unaweza kuweka sukari kiasi. Kumbuka kuwa baadhi ya matunda haya yana sukari hivyo kama si mpenzi usiongeze.

Hadi hapo matunda yako yatakuwa tayari kwa kuliwa,unaweza kuyaweka kwenye kikombe au bakuli maalumu za matunda ili kuleta mvuto. Pia unaweza kutia na ice cream.

 

KUMBUKA. Matunda ni muhimu kwa afya yako, pendelea kula matunda mara kwa mara ili kujipatia vitamin A, C, kuimarisha afya ya macho, kurahisisha mmeng’enyo wa chakula na kuondoa sumu mwilini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles