30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Jinsi MCB inavyowafikia wakulima Mbinga

MCB_Bank_logo.svg (1)

Na AMON MTEGA, MBINGA

WANANCHI wengi wanaofanikiwa kimaisha, wakati mwingine hupata mafanikio hayo baada ya kuzitumia vizuri taasisi za fedha

Wananchi hao wanafanikiwa pale tu wanapokuwa na uhusiano usioyumba na taasisi hizo pindi wanapokopa na kurejesha mikopo yao kwa wakati.

Pamoja na uwepo wa fursa hizo, baadhi ya taasisi za fedha nchini zimekuwa zikishindwa kuwafikia walengwa kwa wakati na hivyo wananchi kushindwa kupiga hatua kupitia sekta ya kilimo, ufugaji na biashara zingine za uzalishaji.

Wakati kukiwa na taasisi za fedha za aina hiyo, wilayani Mbinga, Mkoa wa Ruvuma kuna Benki ya Wananchi Mbinga (MCB), ambayo imekuwa mstari wa mbele kuwafikia wakulima na kuwapa mikopo ya fedha kwa masharti nafuu.

Pamoja na mambo mengine, taasisi hiyo ya fedha inaonyesha nia ya dhati ya kutimiza nia ya Serikali ya awamu ya tano iliyodhamiria kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda.

Akizungumza na MTANZANIA ofisini kwake hivi karibuni, Kaimu Meneja wa MCB, Edwin Namnauka, anasema lengo la benki hiyo ni kuhakikisha uchumi wa mtu mmoja mmoja unakua kupitia mikopo wanayoitoa kwa wananchi.

“Sisi kwetu ni kazi tu kwa sababu tunajua bila kutoa mikopo kwa wananchi Taifa haliwezi kupiga hatua kwani wananchi wanatutegemea pia.

“Kwa mfano, mwaka jana 2015, tulitoa mikopo kwa watu mbalimbali wakiwamo wafanyabiashara wadogo wadogo, wakulima pamoja na baadhi ya vikundi vya kuweka na kukopa.

“Katika mikopo hiyo wafanyabiashara 4,147 walinufaika na tulitumia shilingi bilioni mbili.

“Kwa upande wa vikundi ambavyo ni 828 tulivikikopesha shilingi bilioni 2.6 kwa sababu huko kuna wafanyabishara ndogondogo wapatao 15,365.

“Kuna Saccos nne tulizikopesha shilingi milioni 200 na vicoba tulivikopesha shilingi milioni 106. Kwa takwimu hizo sasa unaweza kuona ni kwa jinsi gani MCB imedhamiria kuwakomboa wananchi katika kipindi hiki ambacho Serikali inajiandaa kuufikia uchumi wa kati,” anasema Namnauka.

Kwa mujibu wa Namnauka, idadi kubwa ya waliokopa wamebadilika kimaisha na sasa wanachangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

“Tuliowakopesha wamebadilika kimaisha kwa sababu baadhi yao walikuwa wakila leo, hawajui kesho watakula nini, lakini baada ya kuwakopesha fedha maisha yao yamebadilika na wana miradi ya kuwaendeshea maisha,” anafafanua Namnauka.

Kuhusu utoaji wa mikopo, meneja huyo anasema walengwa hupewa elimu ili wajue namna ya kutumia fedha watakazokopeshwa.

“Kuna baadhi ya wanaokopeshwa wanahitaji fedha lakini hawana uelewa wa mikopo na hawajui madhara ya kushindwa kulipa mikopo.

“Kwa hiyo, tunachokifanya kwanza ni kujiridhisha kama biashara husika ina leseni, haiharibu mazingira na inatambulika kisheria.

“Baada ya kujiridhisha na sifa hizo tunawapa elimu na kuwaeleza kwa kina faida za mikopo na madhara ya kushindwa kurejesha mikopo yao kwa wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles