27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Jinsi kasisi alivyopanda na kuwa rais

MAHE, SEYCHELLES

KATIKA jaribio lake la sita, Wavel Ramkalawan, kasisi wa Kanisa la Kianglikana, amekuwa Rais wa Seychelles na kumaliza miongo ya upinzani lakini atatakiwa kuliunganisha taifa.

Kulikua na maneno machache ya kuelezea sifa zake katika hotuba ya kuapishwa kwa Ramkalawan alipokuwa akionekana kujikita zaidi katika kuwakaribisha wananchi na wageni wa heshima waliokuwa wameketi katika viwanja vya Ikulu.

“Baada ya miaka 43 tumepata demokrasia, barabara imekuwa ndefu na sasa tutavuna matunda yake.”

Kuchaguliwa kwake ni mwanzo wa mabadiliko kwa visiwa hivyo, ambako urais umekuwa ukitawaliwa na chama kimoja tangu mwaka 1977.

Mbele ya jengo la kifahari la ukoloni la Victoria na gwaride la heshima la jeshi, Wavel mwenye umri wa miaka 58 aliapishwa na Jaji Mkuu Jumatatu.

Rais mpya ni mchungaji aliyetawazwa wa Kanisa la Kianglikana, na haishangazi kwamba ujumbe wake wote ulikua ni wa amani, uvumilivu na wa kuwaomba Waseychelles kufanya kazi pamoja kwa ajili ya umoja wa taifa, na kuzuia mgawanyiko wa miaka mingi sana wa mzozo wa kisiasa.

Akimshukuru rais anayeondoka madarakani, Danny Faure kwa kuyaweka wazi mazungumzo ya kisiasa kwa miaka michache iliyopita, Ramkalawan alisisitizia haja ya kuvumiliana miongoni mwa watu wa Seychelles na akatoa wito wa kile alichokiita kurejea kwa utu miongoni mwa jamii ambapo kila mtu anamsalimia mwenzake habari za asubuhi na ambapo tofauti za asili na kijamii nina wekwa kando.

“Seychelles, inapaswa kuwa mfano wa kuvumiliana kwa dunia nzima. Sisi ni visiwa 115 vidogo katika bahari ya India, lakini hatuna uhusiano mzuri.

“Tutaimarisha mahusiano ya urafiki na nchi zote, na kukaribisha msaada kutoka kwa washirika wetu wa kimataifa wowote watakavyokua,” alisema rais mpya.

‘MWANASIASA WA MADHABAHUNI’

Hili lilikuwa ni jaribio lake la sita, safari ambayo aliianza wakati alipogombea kwa mara ya kwanza wadhifa huo 1998.

Aliingia siasa miaka kadhaa mapema, na alikosolewa na serikali kwa kufanya kile walichokiona kama taarifa ya kisiasa kutoka madhabahuni wakati wa enzi ya chama kimoja.

Alikuwa akikaribia kupata ushindi wa urais mara kadhaa, na mwaka 2015 alishindwa na James Michel kwa kura 193 tu katika awamu ya pili ya upigaji kura.

Akielezea kuhusu miaka yake katika upinzani na kushindwa kwake mara tano katika uchaguzi wa urais, Bw Ramkalawan alitumia nukuu ya Nelson Mandela: “Mshindi ni muotaji ambaye hakati tamaa .”

Licha ya ujumbe mzuri katika hotuba yake ya kuapisgwa, bado kuna migawanyiko ndani ya jamii ya Waseychelles.

Ni miaka 43 tangu visiwa hivyo vilipokabiliwa na ghasia za mapinduzi ya Albert René, ambaye alipindua serikali iliyochaguliwa kidemokrasia James Mancham, mtu aliyeongoza visiwa hivyo kupata uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1976.

Wakati akitoa wito wa amani na utulivu, Rais Ramkalawan alitembelea mchoro wa Gerard Hoarau, mpinzani wa René aliyeuawa mjini London mwaka 1985, na ambaye wauaji wake hawajatambuliwa.

BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles