23.6 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Jill atangaza kujiuzulu kuifundisha Marekani

NEW YORK, MAREKANI

KOCHA wa timu ya taifa ya wanawake ya mpira wa miguu Marekani, Jill Ellis, ametangaza kujiuzulu kuwafundisha mabingwa hao wiki kadhaa baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia nchini Ufaransa.

Kocha huyo anaachana na timu hiyo huku akiwa ameweka historia kubwa kwa taifa hilo baada ya kutwaa taji hilo kubwa duniani mara mbili mfululizo.

Jill alichaguliwa kuwa kocha mkuu mwaka 2014 na kufanikiwa kutwaa mataji nane ikiwa Kombe la Dunia mara mbili, mwaka 2015 nchini Canada na 2019 huko Ufaransa mwezi uliopita.

“Nafasi niliyopata ya kuifundisha timu hii na kufanya kazi na wachezaji waliopo ni kitu cha kujivunia katika maisha yangu.

“Natumia nafasi hii kuwashukuru wachezaji hao kwa kujituma kwao kwa ajili ya taifa na kufanikiwa kutwaa mataji, hata hivyo naweza kusema wamelifanya taifa kuwa kwenye historia ya aina yake kwenye ulimwengu wa soka duniani.

“Ninaamini kwa kile walichokifanya wachezaji hao kitakuwa kinachochea kufanya vizuri zaidi kwa wachezaji wengine wa kizazi kijacho,” alisema kocha huyo.

Hata hivyo, kocha huyo ataendelea kuwa na timu katika ziara ya kufurahia ubingwa wa Kombe la Dunia ambayo itaanza kesho kutwa hadi Oktoba ambapo watacheza jumla ya michezo mitano ya kirafiki.

Baada ya kumalizika kwa ziara hiyo kocha huyo atajiuzulu rasmi, lakini atabaki ndani ya timu hiyo akiwa kama balozi wa mpira wa miguu kwa wanawake nchini Marekani.

Hata hivyo, mkataba wa kocha huyo ulikuwa umalizike baada ya Kombe la Dunia nchini Ufaransa, lakini aliongeza mwingine na kumfanya aendelee kuwa kwenye kikosi hicho hadi 2020 kwenye michuano ya Olympics, hivyo kwa sasa chama cha soka kipo kwenye mipango ya kumtafuta kocha mwingine ambaye atawapeleka kwenye Olympics.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,070FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles