28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Jiko la gesi laripuka ndani ya treni laua watu 70

PUNJAB, PAKISTANI

TAKRIBANI watu 70 wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya jiko la gesi kuripuka ndani ya treni iliyokuwa ikiwasafirisha waumini  waliokuwa wanakwenda kufanya ziara ya kidini kutoka Karachi Pakistan kuelekea Rawalpindi.

Picha za televisheni zinaonyesha moto ukifuka ndani ya mabehewa matatu ya treni huku vilio vikisikika ndani ya treni hiyo katika eneo la vijijini la mkoa wa kati wa Punjab.

Ofisa wa ngazi ya juu wa shirika la safari za reli la Pakistan, Ali Nawaz ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP, kwama baadhi ya abiria-wengi wao wakiwa waumini waliokuwa njiani kwenda katika ziara ya kidini katika mji wa mashariki wa Lahore, walikuwa wakipika chakula cha asubuhi pale majiko yao mawili ya gesi yaliporipuka.

Wapakistan wengi wanabeba vyakula wanapokuwa katika safari ndefu lakini majiko ya gesi yamepigwa marufuku.

Ali Nawaz anasema uchunguzi unafanywa kuhusu ajali hiyo.

Televisaheni za Pakistan zimeonyesha jinsi mamia ya watu walivyokusanyika njiani kuangalia jinsi moto unavyofuka ndani ya mabehewa  ambayo yaliachana na sehemu nyingine ya treni.

Waziri Mkuu, Imran Khan ameamuru uchunguzi juu ya kisa hicho ufanywe mara  moja

Vikosi vya  zimamoto vilifika haraka katika eneo hilo karibu na wilaya ya Rahim Yar Khan. Watumishi wa mashirika ya uokozi na wanajeshi pia walionekana wakisaidia.

Miili ya wahanga wa ajali hiyo iliyofunikwa shuka nyeupe imekuwa ikiondolewa.

“Kwa mujibu wa habari zilizotufikia kutoka eneo la ajali, zaidi ya watu 70 wameuwawa na 40 kujeruhiwa”, waziri wa afya wa mkoa huo Yasmin Rashid aliliambia shirika la habari la AFP.

Majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya mji wa karibu na hapo wa Rawalpindi na miji mingine ya wilaya ya Rahim Yar Khan ameongeza kusema waziri Yasmin Rashid na kuongeza “maiti 18 tu ndizo zilizoweza kujulikkana ni za nani.”

Waziri mkuu Imran Khan ameelezea masikitiko yake kwa yaliyotokea na kuwapa mkono wa pole familia za wahanga pamoja na kuwaombea wapone haraka majeruhi.

Waziri mkuu huyo amesema ameamuru uchunguzi wa kina ufanywe kuhusu kilichotokea.

Vyombo vya habari vinasema baadhi ya abiria wameuwawa walipokuwa wakijaribu kukimbia kutoka ndani ya treni hiyo ambayo ilikuwa ikiendelea kwenda.

Ajali za treni huripotiwa mara kwa mara nchini Pakistan ambapo Julai mwaka huu watu 23 waliuwawa katika wilaya hiyo hiyo pale treni iliyokuwa ikitokea mji wa mashariki wa Lahore ilipogongana na treni ya mizigo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles