24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Jifunze kutoka Exim Bank jinsi ya kukuza biashara yako


Ukuaji katika biashara ni jambo ambalo kila mjasiriliamali angetamani kuliona likitokea katika uwekezaji wake. Ukuaji huo wa kibiashara kwa ujumla wake hutegemea ukuaji na uboreshwaji wa huduma ambazo hutolewa na mfanyabiashara siku hadi siku kwa wateja wake
Exim Bank kama mtoa huduma za kifedha nchini, imeshuhudia ukuaji mkubwa katika sekta ya huduma ambazo imekuwa ikitoa kwa wateja wake kwa miaka 20 sasa toka ilipoanzishwa mnamo mwaka 1997.

Eugen Francis Massawe ambaye ni Mkuu wa operesheni za matawi wa Exim Bank anatoa ufafanuzi juu ya ukuaji wa huduma za Benki hiyo tokea ilipoanzishwa hadi hapa ilipofikia.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=qOuXec2GD3g[/embedyt]

“Nimekuwa na Exim Bank Tanzania Limited kwa kipindi cha miaka 20 sasa kwa kipindi hiki cha miaka 20 nimeshuhudia ukuaji wa huduma zetu mbalimbali. Moja ya huduma hizi ni kurahisisha utumaji wa pesa ambapo ukitaka kutuma pesa nje ya nchi tutatumia muda wa masaa manne tu”. Amesema Eugen Francis Massawe.

Sanjali na huduma hiyo ya kutuma na kutoa pesa nje ya nchi kwa uharaka zaidi, Eugen anaelezea huduma ya kufungua akaunti ndani ya muda mfupi sana.

“Sio hivyo tu, tunafungua akaunti mpya ndani ya masaa sita unapata akaunti yako. Tunarahisha ulipaji wa mishahara ya makampuni mbalimbali kwa muda wa dakika 20 tu”, Anafafanua Eugen.

Kitu cha muhimu na cha kujifunza hapa ni jinsi ya kujali na kuuthamini muda wa mteja wako.  Exim Bank wamekuwa wakilitambua hilo hivyo ukuaji wao umetegemea sana kuwajali wateja wao.

“Kwa kipindi hiki cha miaka 20 nimepata fursa ya kujifunza mambo mengi. Lakini kubwa ni kuwathamini na kuwajali wateja wetu”. Anamalizia Eugen Francis Massawe. Hivyo basi, kama unaendelesha biashara kumbuka kuwaweka wateja wako mbele, mthamini kila mmoja wao na tumia muda mfupi inavyowezekana kuwahudumia.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles