24.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Jezi feki 296 zakamatwa jijini Mwanza

Na Clara  Matimo, Mwanza

 Jeshi la Polisi Mkoa wa  Mwanza linamshikilia Mfanyabiashara, Said Furaha (31) Mkazi wa Nundu kwa tuhuma za kukutwa na jezi feki 296 zenye nembo ya timu za Simba na Yanga kinyume na sheria.

Meneja wa Kampuni ya Vunja Bei Kanda ya Ziwa, Said Malekela, (wa kwanza kushoto) akiangalie jezi feki za timu za Simba na Yanga ambazo zimeshikiliwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhan Ng’anzi (wa kwanza kulia) pamoja na msimamizi wa GSM Tawi la Mwanza, Mahsen Omar, zilizokamatwa kufuatia msako maalumu uliofanywa jijini humo.

Hayo yamebainishwa Julai 13,2022 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhan Ng’anzi, alipozungumza na waandishi wa habari ambapo alifafanua kwamba mtuhumiwa huyo alikamatwa Julai 5, mwaka huu  eneo la barabara ya pamba Sokoni Wilaya ya Nyamagana.

Amesema jeshi la polisi lilipata  taarifa kutoka kwa Afisa Masoko wa kampuni ya GSM na Vunja bei ambao ndiyo wanaosambaza jezi hizo kuwepo kwa mfanyabiashara anayesambaza na kuuza jezi hizo bandia.

Kwa kushirikiana na maofisa kutoka Kampuni ya Vunja Bei ambayo ndiyo inayosambaza vifaa vya michezo kwa ajili ya timu ya mpira ya Simba tulifanikiwa kukamata  jumla ya vifaa vya michezo ikiwemo jezi 145 za club ya Simba.

“Tuliendelea na msako huo ambao ulipelekea kukamata  jezi zingine 151 za club ya Yanga ambazo husambazwa na kampuni ya GSM kutokana na hilo tulifanya uchunguzi wa kina tukaona jezi hizi ni jezi bandia hazikuwa zimesambazwa na kampuni ya vunja bei wala GSM, jezi zote 296 tulizikamata dukana kwa mtuhumiwa,” amesema Kamanda  Ng’anzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhan Ng’anzi, akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) jezi feki za timu za Simba na Yanga ambazo wamezikamata Julai 5, 2022 jijini humo.

Aidha, amebainisha kwamba jeshi la polisi linaendelea kufanya upelelezi wa kina kuhusiana na shauri hilo ili kuweza kubaini mtandao mzima wa wahusika wote wanaotengeneza, kuagiza, kusambaza, kuuza na kuingiza nchini bidhaa hizo bandia ili kuwafikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili kwani wanasababisha wadhamini wa klabu hizo kukosa mapato.

Kwa upande wao Meneja wa Kampuni ya Vunja Bei Kanda ya Ziwa, Said Malekela na Mahsen Omar ambaye ni msimamizi wa  GSM  Tawi la Mwanza, wamelishukuru jeshi la polisi Mkoani Mwanza kwa kushirikiana nao katika msako huo ambao umewezesha kukamata jezi hizo feki pamoja na mtuhumiwa, wameomba  hatua zaidi zichukuliwe dhidi yake ili iwe fundisho kwa wafanyabiashara wengine wenye nia na tabia kama hizo kwani wanapoteza mapato makubwa kwa wadhamini wa timu hapa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles