32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, February 2, 2023

Contact us: [email protected]

‘Jesus’ kortini kwa dawa za kulevya

151221-drugs-stock

Na MANENO SELANYIKA –DAR ES SALAAM

RAIA wa Cape Verde, Liliana Jesus (32), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwa tuhuma za kukamatwa na dawa za kulevya aina ya cocaine yenye uzito wa kilo 2.38 katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA).

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Victoria Nongwa, Wakili wa Serikali, Hellen Mushi, alidai kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Oktoba 18, mwaka huu.

“Mtuhumiwa alikuwa katika harakati za kusafirisha dawa za kulevya aina ya cocaine kutoka hapa nchini ukijua ni kinyume cha sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alidai Wakili Mushi.

Baada ya kusomewa maelezo hayo, mtuhumiwa hakuweza kujibu kitu chochote kwa kuwa haelewi lugha ya Kiingereza wala Kiswahili na Hakimu Nongwa alisema arudishwe mahabusu hadi Desemba 3, mwaka huu shtaka hilo litakapotajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles