Jessie J atarajiwa kuitwa mama

0
1237

LONDON, ENGLANDHATIMAYE nyota wa muziki nchini Uingereza, Jessica Cornish, maarufu kwa jina la Jessie J, amewashtua mashabiki wake baada ya kutangaza kuwa anatarajiwa kuitwa mama.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 30, miaka minne iliyopita aligundulika kuwa na tatizo la kizazi na kudaiwa hataweza kupata mtoto katika maisha yake, lakini sasa inadaiwa kizazi chake kipo salama na anaweza kupata watoto.

“Kwa kipindi cha miaka minne nilikuwa katika maumivu makali na huzuni wa kila siku huku ikiwa siri katika maisha yangu, kwa kuwa niligundulika na tatizo la kizazi na nikaambiwa siwezi kupata mtoto.

“Furaha niliyonayo kwa sasa haielezeki, ninatarajiwa kuitwa mama, ninawashukuru wote ambao walikuwa na mimi katika kipindi hiki kigumu, kweli nimeamini kuna maajabu duniani, nawashukuru sana,” alisema msanii huyo.

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya kumaliza kuimba wimbo wake wa ‘Four Letter Word’ kwenye tamasha la Royal Albert Hall, lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini London.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here