31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Jeshi la Wananchi lamwaga ajira mpya

Kaimu Mkurugenzi waHabari na Uhusiano wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja, GaudenceIlonda, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana kutanga nafasiza kazi  kwa madaktari wa binadamu nafani nyingine za tiba. Kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Ofisi yaUandikishaji wa Jeshi hilo Meja, Lilian Ungani. Picha na Deus Mhagale

Na Mwandishi Wetu– Dar es Salaam

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limetangaza nafasi za ajira kwa madaktari wa binadamu na fani nyingine za tiba.

Nafasi hizo, zimetolewa ili kuongeza idadi ya wataalamu wa tiba watakaotoa huduma za afya katika hospitali za jeshi hilo, vituo vya afya na zahanati kulingana na mahitaji ya sasa na ya siku zijazo.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya ya jeshi hilo, Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano, Meja Gaudence Ilonda alisema watakaondikishwa ni watalaamu wenye taaluma zinaokidhi vigezo.

Meja Ilonda, alisema  watakaoandikishwa kuwa ni wale wenye taaluma ya daktari bingwa wa meno, madaktari bingwa (Specialist Neurasurgeon), mkemia, mteknolojia msaidizi maabara.

Alitaja nafasi nyingine kuwa ni tabibu msaidizi, katibu wa hospitali, msaidizi wa kumbukumbu (Medical Records – Certificate), daktari na ofisa muuguzi.

 “Wengine ni fundi sanifu vifaa tiba (Bio Medical Engineer), tabibu (Clinical Assistant – Certificate), mteknolojia msaidizi (Laboratory Assistant – Certificate), mfamasia (Phamacist – Degree), mtoa tiba kwa vitendo (Physiotherapy – Diploma na Ofisa Muuguzi msaidizi (Assistant Nursing Officer),” alitaja.

Meja Ilonda, alitaja sifa za kuandikishwa jeshini kuwa ni mtu yeyote ambaye ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa, awe na umri wa kati ya miaka 18 hadi 28, isipokuwa kwa wabobezi.

“Awe na afya njema ya mwili na akili timamu, awe mwenye tabia njema, awe hajawahi kupatikana na hatia ya makosa ya jinai mahakamani na kufungwa jela, awe na cheti halisi cha kuzaliwa.

“Vyeti halisi vya shule (Academic and School Leaving Certificates), kama ni daktari awe amemaliza mafunzo kwa vitendo (Internship) na kutunukiwa vyeti pamoja na kusajiliwa na bodi na awe hajatumikia Jeshi la polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo (KMKM),” alisema.

Aliongeza “Wenye sifa hizo na wanaohitaji kujiunga na jeshi hilo waripoti  kambi ya Jenerali Abdallah Twalipo, Mgulani, Dar es Salaam ifikapo Desemba 17, mwaka huu kuanzia saa 1:00 asubuhi kwa usaili.

“Waombaji wafike na vyeti halisi (Orginal Certificates) vyakuzaliwa na masomo, wajitegemee usafiri, chakula na malazi.“Wale watakaochaguliwa na kuandikishwa jeshini watapatiwamafunzo mbalimbali ya jeshi na yatakayowaendeleza katika taaluma yao, wakiwakwenye majukumu watakayopatiwa ni yale yatakayowapa changamoto na fursa nzuriza kutumia taaluma zao,” alisema.M

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles