26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

JESHI LA SUDAN LAMWEKA PAGUMU AL BASHIR

Jeshi la Sudan limeuweka utawala wa Rais wa nchi hiyo Omar al Bashir shakani na limeahidi kutangaza taarifa muhimu wakati wowote kuanzia sasa.

Uamuzi huo wa jeshi, unaashiria kuhitimisha utawala wa muda mrefu wa Bashir

Tayari idadi kubwa ya Wanajeshi wametanda katika makazi rasmi ya Rais tangu asubuhi ya leo, Shirika la Habari la kimataifa la AFP linaripoti.

Mbali na Jeshi kuzingira makazi ya Rais, lakini  pia limeshikilia njia zote muhimu za kuingia na kutoka mji mkuu wa Khartoum.

Magari yaliyosheheni wanajeshi wenye silaha yameegeshwa kwenye barabara zote muhimu na madaraja kwenye mji mkuu, shirika la habari la Reuters linanukuu mashuhuda.

Matangazo ya kawaida ya redio ya Serikali yamekatishwa na kwa sasa zinapigwa nyimbo za ukombozi.

Raia wanaimba kwa furaha, “serikali imeangushwa. Tumeshinda,” shirika la Reauters linaripoti.

Maelfu ya watu wako barabarani wakijaribu kuelekea makao makuu ya wizara ya Ulinzi kuungana na waandamanaji ambao wamekuwa wakishinikiza Rais Bashir kubwaga manyanga baada ya miaka 30 madarakani.

Waandamanaji hao wamekaidi mabomu ya kutoa machozi kutoka kwa vikosi vya usalama tangu walipoanza kupiga kambi katika eneo hilo mnamo Aprili 6.

Maafisa wanasema watu 49 wameuawa katika machafuko yanayohusiana na maandamano hayo tangu yalipozuka Desemba mwaka jana.

Marekani kwa mara nyingine imerudia wito wake kwa Serikali kuruhusu maandamano ya amani. Jeshi la polisi la Sudan limewaamuru maafisa wake kutoingilia kati maandamano hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles