25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Jeshi la Polisi Tanga laimarisha ulinzi

OSCAR ASSENGA,TANGA.

Jeshi la Polisi Mkoani Tanga , limesema limejipanga kuimarisha ulinzi ikiwemo kuendesha misako mbalimbali na doria wakati wa sikukuu ya Eid El Fitr itakayofanyika mkoani hapo ili kuhakikisha inasheherekewa kwa usalama na amani bila bugudha huku likitoa katazo kwa wananchi kuacha kuogelea kwenye maeneo yasiyokuwa rasmi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 31, Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Edward Bukombe amesema yeyote atakayekiuka maagizo hayo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Bukombe ametoa angalizo kwa wamiliki wa maeneo ya starehe ikiwemo hotel, bar na sehemu nyengine za Starehe ikiwemo kumbi za mziki usiku (Night Club) kuzingatia muda wa kufungua na kufunga kwa mujibu wa sheria za nchi na amewataka wazazi,walezi kuwa makini na usimamizi na uangalizi wa watoto nakusema itasaidia kuepukana na changamoto ya kupotea kwao .

“Lakini pia napenda kutoa angalizo kwa wananchi wote wa Tanga kuhakikisha wanakuwa waangalifu kwa usalama wao wenyewe na mali zao hii ni kwa kuwa kila mtu anapaswa kuzingatia usalama wake kwanza…kila wanapotoka  nyumbani kuelekea misikitini kuswali au katika maeneo ya starehe anapaswa kuhakikisha ameacha ulinzi wa kutosha katika makazi yake kuepuka kuibiwa mali yake ,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles