27.2 C
Dar es Salaam
Monday, January 20, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Jeshi la Polisi Mara laokoa wasichana 100 ukeketaji

Na Malima Lubasha, Mara

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Kipolisi Tarime na Rorya mkoani Mara, limefanikiwa kuwaokoa wasichana zaidi 100 waliokuwa wanatarajiwa kukeketwa katika msimu wa ukeketaji unaoendelea katika wilaya za Tarime/Rorya.

Wasichana hao wameokolewa na kupelekwa katika nyumba salama iliyoko katika kituo cha Kanisa Katoliki Masanga kinachopinga ukeketaji wilayani Tarime kuanzia Desemba 3 ,2024 hadi sasa kufuatia oparesheni maalum inayofanywa na jeshi hilo kwa ajili ya kuwanusuru watoto

Taarifa hiyo imetolewa Desemba 9, 2024 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Tarime/Rorya, Mark Njera kwenye maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo amesema koo tisa kati ya 12 za Wakurya katika kanda hiyo zinafanya tohara mwaka huu kwa mujibu wa mila desturi zao.

Kamanda Njera amesema ukeketaji unafanyika katika musimu wa tohara na kwama kutokana na koo nyi ngi kufanya tohara mwaka huu,jeshi hilo liliona kuna haja ya kuongeza nguvu zaidi ili kuwanusuru wato to wa kike ambao wapo katika hatari ya kukeketwa katika msimu huu wa tohara ambao tayari umeanza.

“ Jeshi la Polisi Makao Makuu limekubaliana na sisi na kutuongezea nguvu askari 150 ambao walifika kwenya mkoa wa Tarime/Rorya tangu Desemba mosi mwaka huu na kuanza kaziDesemba 3 hadi sasa na tumefanikiwa kuwaokoa wasichana zaidi 180 waliokuwa katika hatari ya kukeketwa,”amesema kamanda Njera

Kamanda Njera amesema askari hao kwa kushirikiana na wengine wa kanda maalum wanaendelea kutoa elimu juu ya madhara ya ukatili ikiwepo ukeketaji pamoja na kuendesha doria za oparesheni maalum ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya ukeketaji wa vitendo vya ykatikli wa kijinsia kwa ujumla.

Amesema kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika eneo hilo vinaendelea kupungua kutokana na sababu mbalimbaliikiwemo jitihada zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau kwa kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya ukeketeji na ukatili wa kijinsia.

Kamanda Njera alifafanua kuwa ili kumaliza kabisa vitendo hivyo vya ukeketaji ipo haja ya serikali kutu nga sheria maalum inayohusu ukeketaji,tofauti na sasa ambapo sheria inayotumika ina upungufu mwing I hali ambayo kwa namna moja ama nyingine imekuwa ukichangia kuendelea kwa vitendo hivyo vya uke ketaji.

“ Kuwepo na madawati ya kijinsia katika kila kituo cha Polisi ili iwe rahisi kushughulika na vitendo hivi kwa wakati na pia serikali ijenge nyumba salama na kufungua vituo jumuishi katika kila wilaya ili kurahisi sha huduma kwa waathirika na manusura wa ukeketaji,”amesema Njera

Amesema mwaka huu 2024 jumla ya matukio 1,099 yanayohusu ukatili wa kijinsia yameripotiwa ikilinganishwa na mwaka jana kwa kipindi kama hiki ambapo jumla ya matukio 1,163 yaliripotiwa hapa tunaweza kuona matukio yamepungua kwa asilimia 5.8 na juhudi bado zinahitajika kuendelea.

“ Elimu imetolewa kwa wanafunzi wa shule za msingi wapatao 13,000,shule za sekondari wanafunzi 11,000,watu wazima 96,kata 60,minada,makanisa,na vikundi ambapo katika kipindi hicho wasichana zaidi 113 waliokolewa katika hatari ya kukeketwa ,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles