29 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Jeshi la Polisi lashtukia njama za Chadema kuvamia vituo vya polisi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Jeshi la Polisi Tanzania limeonya vikali dhidi ya mipango inayodaiwa kufanywa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa lengo la kuhamasisha vurugu na kuvuruga amani ya nchi. Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, ametoa kauli hiyo leo, akisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayejihusisha na vitendo hivyo.

Misime amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kutoa elimu kwa Watanzania, wakiwemo wanasiasa, juu ya umuhimu wa kulinda amani na utulivu wa nchi kama msingi wa maendeleo. Ameeleza kuwa badala ya kupanga njama za vurugu, ni muhimu kwa kila raia kuzingatia sheria na kuchangia katika ujenzi wa taifa.

“Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa yeyote atakayeendelea kuratibu, kuhamasisha, au kushiriki katika mipango ya kuvuruga amani ya nchi yetu. Wale watakaobainika kufanya hivyo watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi,” alisema Misime.

Onyo hilo linakuja wakati ambapo Jeshi la Polisi linafanya jitihada za kuimarisha ulinzi na usalama wa taifa, huku likiwataka wananchi kushirikiana na vyombo vya dola katika kudumisha amani, badala ya kushiriki katika njama za kuleta vurugu ambazo zinaweza kuhatarisha maendeleo ya nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles