33.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, March 22, 2023

Contact us: [email protected]

Jeshi la polisi laendelea kukuna vichwa uchunguzi wa Mo

Bethsheba Wambura, Dar es SalaamLicha ya kupatikana akiwa hai baada ya kutekwa kwa siku 9 kwa mfanyabiashara na mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji maarufu Mo, Jeshi la Polisi nchini linaendelea kukuna vichwa kuchunguza tukio hilo.

Mfanyabiashara huyo alitekwa alfajiri ya Oktoba 11, mwaka huu na watu wasiojulikana akiwa katika Hoteli ya Colloseum Oysterbay jijini Dar es Salaam, wakati akiingia kufanya mazoezi hotelini hapo na kupatikana Oktoba 20, mwaka huu baada ya kutupwa katika viwanja vya Gymkhana.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumanne Novemba 6, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Liberatus Sabas amesema jeshi hilo liachwe lifanye kazi yake na litakapomaliza litatoa taaifa rasmi ya wapi wamefikia katika uchunguzi wao.

“Kuhusu tukio la kutekwa Mo Dewji, watu wajue kufanya uchunguzi ni mchakato mrefu inachukua muda kujua ni nani aliyefanya na yuko wapi kwa sasa, tutakapokuwa na taarifa mpya tutawatoa ili mjue maendeleo ya uchunguzi wa tukio hilo,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,079FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles