31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Jerry Medard: Mkongomani aliyejiongeza na kuwa Mc Marekani

KENTUCKY, MAREKANI

KARIBU katika safu hii ya Nje ya Box, ambayo inakuletea mada na makala mbalimbali zitakazokufanya ufikiri kwa upana huku ukipewa mwangu wa kutazama mambo kwa jicho la tatu.

Jerry Medard ni  miongoni mwa vijana waliojiongeza na kufanikiwa kuwa mshereheshaji (MC) pendwa kwenye Mji wa Louisville, Kentucky nchini Marekani baada ya kumaliza chuo cha Columbus Technical College mwaka 2012.

Akizungumza na safu hii, Jerry  ambaye alizaliwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kukulia Mkoa wa Kigoma, Tanzania mwaka 1999 kabla hayakwenda Marekani, anasema alipoingia nchini humo alipata usumbufu wa kutokuwa karibu na Waafrika wanaozungumza Kiswahili.

“Wengi niliowakuta walikuwa wanatoka Uganda, Malawi, Burundi, Rwanda na Somalia. Mwaka 2012 nilifanya kazi na nikawa na hamu ya kusoma kwahiyo nilikwenda chuo na baada ya kumaliza nikawa nafikiria nitafanya kitu gani kwa sababu bado nilikuwa na mambo ya ujana, mama akawa amenikumbusha kwamba nina vipaji mbalimbali pia familia yangu ni watu wa imani ni walokole wa Pentekoste.

“Nikajikuta nina wito wa kumtumikia Mungu hapa Marekani na ilipofika 2017 nikapata maono ya kuanzisha kanisa langu nikishirikiana na shirika moja  la kiimani ambalo lipo Tanzania, Afrika Kusini, Kongo DRC, Rwanda  na nchi nyingi na mpaka sasa hivi ninaendelea kama Muinjilisti na Katibu wa kanisa,” anasema.

Anasema aligundua ana nguvu ya ushawishi wa kuongea jambo na watu wakamsikiliza na kufurahi hivyo alitumia nafasi hiyo kuingia kwenye sanaa ya ushereheshaji.

“Nilipata pia maoni kutoka kwa wazee wakaniambia Jerry una kitu ndani yako, na hicho kitu ni usemaji wako maana unaposimama mbele za watu wazima, viongozi watu wanakuwa makini kukusikiliza na kukuamini, hapo nikajua kwamba ninakubalika kwa asilimia 97, hapo nikapata hilo wazo la kuingia kwenye tasnia ya ushereheshaji.

“Mara ya kwanza kuwa MC nilikwenda nje ya Kentury kufungisha ndoa, nilipofika kule harusi ilikuwa nzuri ila watu waliotakiwa wasimamie hawakuwa tayari, mimi nikaenda kwa watumishi wa Mungu wenzangu nikawaambia hayo madhaifu, nilikuwa sijaandaliwa, niliwaongoza maharusi vizuri mpaka kwenye madhabahu ndoa ikabarikiwa kisha tukaenda ukumbini, tukakuta mambo mabaya, ikabidi waniombe tena nisimamie na pale, nikubali kusimamia mwanzo mpaka mwisho kama Mc, nikafanyavizuri na baada ya hapo watu wengi walichukua namba zangu, wakitaka huduma yangu,”

Jerry anasema katika jamii wa waafrika hakukuwa na kitu kama Mc, hivyo yeye aliamua kutumia fursa hiyo kuanzisha kampuni ya ushereheshaji ambayo mpaka sasa inafanya vizuri nchini Marekani.

“Nilipata maono ya kuwa Mc kwa sababu kwenye jamii ya watu wanaozungumza Kiswahili hakukuwa na kitu kama hicho,” anasema Jerry.

Akaongeza kuwa maandamano ya watu weusi pamoja na corona kutikisa Marekani, kumrudisha nyuma kwa sababu kazi yake inahusisha watu wengi.

“Corona imeathiri vitu vingi sana kwenye maisha yetu binafsi, mimi nilikuwa nina harusi mbili nilizotakiwa kusisimamia kabla ya corona ambazo zilisitishwa pia kazi zote kwenye kampuni zilisimamishwa kwa upande wa George Floyd mimi imeniathiri kwa asilimia ndogo ila kwa Wamarekani weusi wazawa ndio wameathirika,” anasema.

Akizungumzia Mc maarufu waliomvutia zaidi kufanya kazi hiyo, Jerry anasema: “Napenda na kutamani, waafrika huku tunavyoishi ni kwamba Wakongomani wakiwa na harusi wanajitafuta wenyewe na Watanzania wakiwa na sherehe wanajitafuta wenyewe kwahiyo ningetamani na kwa sababu napenda Tanzania ndio nchi niliyokulia kuna Mc wazuri ambao nawakubali Mc Luvanda napenda sherehe zake na Mc Pilipili naye napenda maneno yake anapofanya kazi ningetamani tushirikiane siku moja.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles