27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Jenista ataka miundombinu  kuzuia mafuriko Dar

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM



WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama ametoa maagizo matano kwa kamati ya usimamizi wa menejimenti ya maafa ya Mkoa Dar es Salaam.

Mhagama alitoa maagizo hayo jana alipofanya ziara ya siku moja mkoani Dar es Salaam kwa lengo la kukagua miundombinu ya kukabiliana na maafa ya mafuriko pamoja na kutaka kujua mikakati ya kamati ya usimamizi wa menejimenti ya maafa mkoani humo.

Katika maagizo hayo, Mhagama aliitaka Kamati hiyo kusimamia suala la uharibifu wa mazingira hususani maeneo ya mito na mabondeni kwa mujibu wa sheria ya menejimenti ya maafa ya mwaka 2015.

Katika ziara hiyo Waziri Mhagama elitembelea wilaya zote za Mkoa wa Dar es salaam ambazo zimeboresha miundombinu ya kukabiliana na maafa ya mafuriko.

Maeneo hayo ni Jangwani, Mto Mbezi, Mto Ng’ombe, Mto Bungoni na mfereji wa Mtoni Kwa Azizi Ally.

“Nimeridhishwa na juhudi zilizofanywa na serikali kuu chini ya uongozi wa Dk John Magufuli za kuboresha miundombinu ya kakabiliana na maafa ya mafuriko na nimeona jinsi serikali ya ngazi ya mkoa na wilaya zote zinavyo jitahidi kujenga uwezo  wa kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na maafa.

Aidha alifafanua kuwa maafa mengi ya mafuriko mkoani humo yanatokana na uharibifu wa mazingira unaochangiwa na  ujenzi  katika maeneno yasiyo stahili kama kingo za mito na mabondeni.

Aidha Mhagama ameitaka kamati hiyo  kusimamia suala la usafi wa mitaro, mifereji na mito iliyopo  jijini  Dares salaam, ambayo hujaa maji wakati wa msimu wa mvua kutokana  na uchafu na takataka zilizotupwa katika mifereji na mitaro hiyo.

Awali akieleza mikakati iliyopo ya kukabibiliana na maafa katika mkoa wa Dar es salaam, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema mkoa wake umekuwa ukitumia fedha nyingi wakati wa kurejesha hali ya miundombinu iliyoathirika kutokana na maafa ya mafuriko ambapo kwa mwaka 2011 Sh bilioni 4.5 zilitumika kurejesha miundo mbinu ya barabara zilizoharibika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles