27.8 C
Dar es Salaam
Monday, December 6, 2021

Jengo Tume ya Uchaguzi Nigeria lateketea kwa moto

LAGOS, Nigeria

JENGO la Tume ya Uchaguzi nchini hapa, limeteketea moto zikiwa ni takriban siku sita kabla ya kufanyika  uchaguzi mkuu.

 Kwa mujibu wa msemaji wa tume hiyo, jengo hilo ambalo lipo katika Jimbo la  Plateau liliteketea jana na kuunguza vitu vyote muhimu katika uchaguzi huo yakiwamo makasha na karatasi za kupigia kura.

Msemaji huyo alisema  njama hizo ni kutaka kukwamisha shughuli hiyo ya upigaji kura, lakini akakaririwa na gazeti la This Day akisema   bado ni mapema kuwatuhumu wahusika.

Uchaguzi huo mkuu unatarajiwa kufanyika Jumamosi ijayo na jana Rais  Muhammadu Buhari alionya kuhusu kuwapo  vitendo vya rushwa.

 Katika hatua nyingine, Mshirika mkuu wa Rais  Muhammadu Buhari katika uchaguzi mkuu ujao nchini hapa, amewatishia raia wa kigeni akisema  yeyote ambaye atajaribu kuingilia mchakato huo atarejeshwa nyumbani kwao akiwa ndani ya mfuko wa kuhifadhia maiti.

Nasir El-Rufai,ambaye ni Gavana wa Jimbo la  Kaduna,alitoka  kauli hiyo juzi katika mahojiano na Kituo cha Televisheni ya Taifa  ilipoanzishwa mada kuhusu jukumu la jumuiya za kimataifa katika uchaguzi huo.

Mada hiyo iliibuka kutokana na kuwapo  kelele za jumuiya za kimataifa  kutoka Juamuiya ya Umoja wa nchi za Ulaya (EU), Marekani na Uingereza kuhusu kusimamishwa kazi  Jaji Mkuu,  Walter Onnoghen  kwa tuhuma za kuvunja kanuni za utawala bora.

“Tunamsubiri mtu yoyote ayakayejitokeza na kuingilia uchaguzi atarejea nyumbani akiwa kwenye mfuko wa kuhifadhia maiti kwani hakuna aliyekuja Nigeria na kutelekeza jinsi ya kuendesha nchi yetu,”alisema  El-Rufai katika mahojiano hayo kuhusu uchaguzi huo wa Februari 16 mwaka huu.

“Tulipata uhuru wetu na tunajaribu kuiendesha nchi yetu vizuri kadri iwezekanavyo,”aliongeza gavana huyo.

Uchugazi huo katika taifa hilo ambalo ni wazalishaji wakubwa wa mafuta unawakutanisha Rais Buhari ambaye aliingia madarakani mwaka  2015 na kiongozi mkubwa wa upinzani,  Atiku Abubakar ambaye ni makamu wa rais   wa zamani.

Ushindano wao unaonekana kuongeza katika   wiki chache zilizopita.

Mwaka jana  viongozi hao wawili walisaini makubalino yanayoonyesha   watajitolea   kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa amani.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,340FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles