26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Jengo la Mama na Mtoto Mwanza lafikia asilimia 70

Na Yohana Paul, Mwanza

Mradi wa jengo la mama na mtoto katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou-Toure lenye urefu wa ghorofa tano ulioanza kujengwa oktoba mwaka 2017 hadi sasa umefikia asilimia 70 mpaka kukamilika.

Hayo yalielezwa wiki ikiyopita na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou-Toure, Dk. Bahati Msaki wakati akisoma taarifa ya maendelo ya mradi huo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima akiwa ziarani mkoani hapa.

Dk.Bahati alisema ujenzi huo unatarajiwa kugharimu Sh.bilioni 10.1 hadi kukamilika na inatarajiwa kuwa na uwezo wa kuchukua vitanda 261 kusaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

Kwa upande wake Kaimu Meneja  Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mhandisi Moses Urio alisema  kutokana na eneo hilo kuwa na maji  kulipelekea msingi kujengwa kwa muda mrefu  na kuboreshwa kwa mahitaji,  kubadilika kwa mchoro ambapo vitanda  viliongezeka kutoka  100 hadi 261.

Aidha, Dk. Gwajima alimtaka mkaguzi wa majengo ya serikali kusimamia miradi huo kuhakikisha unakamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma za matibabu na kusisitiza ni vema wakandarasi wa miradi  mbalimbali ya  afya kufanya vikao na wajumbe ili kubadilishana  mawazo wakati wa utekelezaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya nyamagana, Dk. Philis Nyimbi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella  alisema  atahakikisha anafatilia kwa karibu ujenzi huo ili uweze kukamilika kwa wakati na wananchi waweze kupata matibabu kwenye jengo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles