23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Jenerali Ulimwengu anusurika kwenda jela

MWANDISHI wa habari mkongwe nchini, Jenerali Ulimwengu.
MWANDISHI wa habari mkongwe nchini, Jenerali Ulimwengu.

Na Maneno Selanyika, Dar es Salaam

MWANDISHI wa habari mkongwe nchini, Jenerali Ulimwengu (68), amenusurika kwenda jela miezi sita baada ya kulipa faini ya Sh 50,000 kutokana na kosa la kusababisha ajali barabarani.

Mbele ya Hakimu Issa Kasailo wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kinondoni, Wakili wa Serikali, Matarasa Maharagande alidai kwamba mtuhumiwa huyo alisababisha ajali hiyo Agosti 26 mwaka huu katika makutano ya barabara ya Kaunda na Ally Hassani Mwinyi Manispaa ya Kinondoni.

Alidai mtuhumiwa anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kusababisha ajali na kumsababishia majeraha Irfan Merali, kutokana na kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha uharibifu wa magari mawili.

Alidai kuwa mshtakiwa akiwa dereva wa gari lenye namba za usajili T640 BEX  Mercedes Benz aliendesha katika barabara ya umma bila kuchukua hadhari ambapo alikatisha na kisha kugonga gari nyingine yenye namba za usajili T 470 DDS Subaru Preza ambapo baada ya kugonga gari hilo alimsababishia maumivu mtu aitwaye Irfan Montazir Merali aliyekuwa dereva.

Baada ya maelezo hayo mtuhumiwa alikiri kosa ambapo mahakama ilimtia hatiani kwa makosa hayo.

Kutokana na hatua hiyo, Mahakama ilimtaka mshtakiwa kulipa faini ya Sh 50, 000 au kwenda jela miezi sita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles