25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Jenerali Tumukunde ashtakwia rasmi kwa uhaini

KAMPALA, UGANDA

MAHAKAMA ya Kampala imeagiza mtia nia ya kuwania urauis wa Uganda, Luteni Jenerali Henry Tumukunde kurejeshwa katika gereza la Luzira hadi Machi 30 kwa tuhuma za kumiliki bunduki kinyume cha sheria na uhaini.

Akitoa agizo hilo katika ukukmbi wa Mahakama ya mjini KampL juzi, Hakimu Mkazi, Valerian Tuhimbise alishauri Tumukunde asijibu chochote kwa kuwa korti hiyo haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Jenerali huyo mstaafu anakabiliwa na mashtaka ya uhaini na umiliki wa bunduki kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa karatasi ya mashtaka, Lt. Jenerali Tumukunde aliyestaafu mnamo Machi 13, 2020 huko Impala Avenue Kololo jijini Kampala alikuwa na bunduki ya AK-47 iliyorekebishwa lakini hakuwa na cheti halali cha silaha.

Tumukunde ambaye alionekana mwenye sura dhaifu aliingizw andani ya mahakama kwa kusaidiwa na maofisa wa usalama kwani hakuweza kutembea mwenyewe.

Jamaa wa karibu wa mkuu huyo wa jeshi aliyestaafu alisema alichukuliwa kutoka katika Hospitali ya Kololo kufuatia kudondoka alipokuwaakishikiliwa na polisi tangu Jumatatu.

Tumukunde, ambaye pia ni waziri wa zamani wa ulinzi na usalama, alikamatwa wiki iliyopita baada ya kudaiwa kutoa maeno yanayoashiria uhaini.

“Kukamatwa kwake kunafuatia matamshi yake katika mfululizo wa mahojiano ya redio na televisheni, ambayo yanadaiwa kuchochea chuki ambazo zinaweza kusababisha uhasama wa watu, kuchochea na kutukuza vurugu kwa jumla. Kwa kuongeza, anataka kuungwa mkono na nchi jirani ili kumuunga mkono katika kuondoa uongozi wa sasa na au bila kura,” msemaji wa Polisi, Fred Enanga alisema awali.

Wakati huo huo, watu wengine 11 waliokamatwa na Tumukunde wameshtakiwa kwa kizuizi cha haki kwa kuzuia Sgt Michael Akello na D / ASP Richard Mwesigwa mnamo Machi 12 na 13, 2020 ambao waliripotiwa kufanya uchunguzi wa halali wa kubaini vifaa katika ofisi binafsi ya Jenerali Tumukunde huko Kololo .

Mbunge Mwanamke wa Tororo Annet Nyakecho na ndugu wa Tumukunde, Arthur Kiiza ni kati ya wale 11 aliokamatwa na kushtakiwa.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,526FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles